Monday, 4 December 2017

Rais wa zamani wa Yemen Abdullah Saleh 'auawa'

Picha ya Ali Abdullah Saleh akihutubu Sanaa, Yemen (24 August 2017)
Haki miliki ya pichaEPA
Image captionAli Abdullah Saleh alikuwa mshirika wa wapiganaji wa Houthi vita vilipozuka 2015
Aliyekuwa rais wa Yemen Ali Abdullah Saleh ameuawa katika mapigano na washirika wake wa zamani, taarifa zinasema.
Mashirika ya habari yanayodhibitiwa na waasi wa Houthi yamewanukuumaafisa wakitangaza "mwisho wa mzozo wa wanamgambo wahaini na kiongozi wao".
Duru katika chama chake Bw Saleh cha General People's Congress pia wamethibitisha kwamba amefariki, kwa mujibu wa Al Arabiya TV.
Picha na video zilizosambazwa mtandaoni zimeuonesha mwili wa mwanamume anayefanana na Bw Saleh ukiwa na kidonda kichwani.
Hadi kufikia wiki iliyopita, wafuasi wa Bw Saleh walikuwa wanapigana pamoja na wapiganaji wa jamii ya Houthi dhidi ya rais wa sasa wa Yemen Abdrabbuh Mansour Hadi.
Lakini uhasama wa muda mrefu wa kisiasa pamoja na mzozo kuhusu udhibiti wa msikiti mkuu katika mji mkuu wa Sanaa unaodhibitiwa na waasi vilichangia mapigano makali ambayo yalisababisha vifo vya watu zaidi ya 125 na wengine 238 kujeruhiwa tangu Jumatano usiku.
Jumamosi, Bw Saleh aliahidi "kufungua ukurasa mpya" na Bw Hadi anayesaidiwa na muungano wa mataifa yanayoongozwa na Saudi Arabia iwapo majeshi hayo yangeacha kuishambulia Yemen na kuondoa marufuku ya kutoingiza chakula na bidhaa Yemen.
Pande hizo mbili zilipokea kwa furaha tamko la Bw Saleh.
Lakini waasi wa Houthi walitazama hilo kama "mapinduzi" dhidi ya "ushirika ambao hakuwahi kuwa na imani nao."
Watu zaidi ya 8,670 wameuawa na wengine 49,960 kujeruhiwa tangu majeshi ya muungano unaoongozwa na Saudi Arabia yalipoingilia kati vita vya wenyewe kwa wenyewe Machi 2015, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.
Mzozo huo pamoja na marufuku ya kutoingiza chakula na bidhaa Yemen ambayo imekuwa ikitekelezwa na Saudi Arabia pia umewaacha watu 20.7 milioni wakihitaji kwa dharura msaada wa kibinadamu, na pia kusababisha hitaji kubwa zaidi ya chakula cha dharura duniani.
Aidha, kulitokea mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ambao unaaminika kusababisha vifo vya watu 2,211 tangu Aprili

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search