Friday, 22 December 2017

RAMSEY NOAH AZURU KABURI LA KANUMBA NA KUNENA HAYA MAZITO

Ramsey Noah Azuru Kabuli la Kanumba Asema  "Aliondoka Kipindi Nyota Yake ya Mafanikio Ikianza Kung'aa"


NGULI wa filamu za Nigeria, Ramsey Noah amesema japokuwa miaka mingi imepita tangu kufariki dunia kwa aliyekuwa msanii mahiri wa filamu za Kibongo, Steven Kanumba, bado pengo lake haliwezi kuzibika katika ulimwengu wa tasnia ya filamu.

Akizungumza katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam alikoenda kuzuru kaburi la marehemu Steven Kanumba leo Jumamosi, Desemba 16, 2017, Ramsey, alisema Kanumba aliondoka kipindi ambacho nyota yake ya mafanikio ndiyo kwanza ilikuwa imeanza kung’ara na kwamba, kila anapomkumbuka na mambo waliyoyafanya pamoja, huwa haamini kama hatamuona tena maishani mwake

Ramsey alizuru hapa nchini kuhudhuria Tamasha la Kutambua Fursa kwa vijana lilioandaliwa chini ya Kampuni ya Sahara, tamasha hilo lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), juzi Alhamisi.

Katika kuzuru kaburi hilo  aliongozana na mama mzazi wa marehemu Kanumba, Flora Mtegoa, mdogo wa marehemu, Seth Bosco, wasanii wa filamu na mashabiki wa marehemu Kanumba.

Ramsey ndiye msanii wa kwanza mkubwa nchini Nigeria kufanya filamu na Mtanzania ambapo walifanya Moses na Devil’s Kingdom jambo ambalo liliunganisha Bongo Movie na Nollywood hivyo kutengeneza uhusiano imara kati ya nchi hizi mbili katika tasnia ya filamu.

Kanumba alifariki dunia Aprili 7, 2012 baada ya kutokea mzozo kati yake na aliyekuwa mpenzi wake, muigizazi Elizabeth Michael ‘Lulu’. Mwanadada huyo kwa sasa anatumiankifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na ya kumuua Kanumba bila kukusudia.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search