Monday, 4 December 2017

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI NEC YATANGAZA UCHAGUZI WA MARUDIO KATIKA JIMBO LA SINGIDA KASKAZINI, LONGIDO NA SONGEA MJINI NA KATA SITA

National Electoral Commission (Tanzania) Logo.png
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza ratiba ya uchaguzi mdogo katika majimbo ya Singida Kaskazini, Longido na Songea Mjini na kata sita za Tanzania Bara ambao utafanyika Januari 13 mwakani.


Akitoa taarifa kwa umma jijini Dar es Salaam leo Jumamosi, Makamu Mwenyekiti wa NEC, Jaji mkuu mstaafu wa Zanzibar, Hamid Mahmoud Hamid amesema tume imetangaza uchaguzi huo baada ya kupokea barua kutoka kwa Spika ya kwamba nafasi ziko wazi.

Jimbo la Singida Kaskazini liko kutokana na kujivua uanachama wa CCM aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Lazaro Nyalandu, Songea Mjini baada ya kifo cha Leonidas Gama na Longido baada ya Mahakama kufuta matokeo ya uchaguzi yaliyokuwa yamempa ushindi Onesmo Ole Nangole.

Akizungumzia uchaguzi wa kata sita amesema waziri mwenye na serikali za mitaa kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, aliitaarifu Tume kuwepo nafasi wazi za madiwani katika kata hizo Tanzania Bara.

Alizitaja kata zinazohusika katika uchaguzi huo kuwa ni Kimandolu(Arusha), Kihesa (Iringa), Bukumbi (Uyui), Kurui (Kisarawe), Keza (Ngara) na Kwagunda (Korogwe).

Amesema utoaji fomu za uteuzi katika majimbo hayo na kata hizo sita utakuwa ni kati ya Desemba 12 hadi 18, 2017 wakati katika jimbo la Songea Mjini utoaji fumo utakuwa kati ya Desemba 14 hadi 20 mwaka huu.

Alifafanua kuwa kwa upande wa kampeni za uchaguzi huo katika majimbo ya Singida Kaskazini na Longido na kata zote sita zitaanza Desemba 19 na kumalizika Januari 12. 

Katika jimbo la Songea Mjini, amesema kuwa kampeni za zitaanza tarehe 21 Desemba, 2017 na kumalizika tarehe 12 Januari, 2018 wakati siku ya uchaguzi katika majimbo yote matatu na kata zote sita itakuwa tarehe 13 Januari, 2017.

Jaji Hamid alivikumbusha vyama vya siasa na wadau wote wa uchaguzi wazingatie sheria, kanuni, taratibu, miongozo na maelekezo yote wakati wa kipindi cha uchaguzi mdogo wa majimbo hayo na kata sita.
Chanzo-Mwananchi

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search