Saturday, 23 December 2017

UVCCM NAO WAUNDA KAMATI KUFUATILIA MALI ZAO NA VITEGA UCHUMI VYAO

Umoja wa Vijana UVCCM, umeunda kamati ya kufuatilia vitega uchumi na mali za umoja huo nchi nzima. 

Kamati hiyo inaundwa na wajumbe nane na itaongozwa na Mariam Chaurembo.


Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka amesema kamati hiyo inakwenda kuchunguza na kuangalia vitega uchumi na mali zote za umoja huo.


"Mwenyekiti ameanza na kazi hii ili aweze kujua mali na vitega uchumi na umoja viko katika hali gani na vinaendeshwaje,"


"Wajumbe hawa watafanya kazi hiyo kuanzia leo wakiangalia na kufuatilia, kuchunguza, kuorodhesha mali za chama na mapato yanayotokana na vitega uchumi hivyo zinakwenda wapi," amesema Shaka


Wajumbe wengine wa kamati hiyo ni Peter Kasera, Zelote Saitoti, Rose Manumba, Sofi Kizigo na Elly Ngowi. Shaka amesema wajumbe wengine wawili watateuliwa kujiunga na kamati hiyo ambayo inaanza leo.

Na Elizabeth Edward,Mwananchi

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search