Monday, 18 December 2017

ZANZIBAR YASHINDWA KWA PENATI, KENYA YATWAA UBINGWA WA CHALENJIKikosi cha Zanzibar Heroes

Ubingwa huo umepatikana baada ya matokeo ya mabao 2-2 katika dakika 120, awali timu hizo zilimaliza dakika 90 zikiwa sare ya mabao 1-1.
Kenya ndiyo iliyoanza kupata bao la kwanza kupitia kwa Ovella Ochieng kisha Zanzibar ikasawazisha baadaye mfungaji akiwa ni Khamis Mussa Makame.

Katika dakika 30 za nyongeza Kenya ikaongeza la pili kupitia kwa Masudi Juma kisha Zanzibar wakapambana na kufanikiwa kusawazisha mfungaji akiwa yuleyule, Khamis Mussa Makame.

Katika mchezo huo kipa wa Kenya, Patrick Matasi ndiye aliyekuwa shujaa kwa kupangua penati tatu za Zanzibar katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Kenyatta mjini Machakos.

Wachezaji wa Zanzibar waliokosa penati ni Adeyoum Ahmed, Issa Haidari ‘Dau’ na Mohammed issa ‘Banka’ huku mbili tu za viungo Feisal Salum Abdallah na Mudathir Yahya Abbas zikijaa wavuni.
Upande wa kipa wa Zanzibar, Mohammed Abulrahman alipangua mikwaju ya Duncan Otieno, wakati za Joackins Atudo, Wesley Arasa Onguso na Samuel Onyango walifunga.
Kikosi cha Zanzibar Heroes
Mohammed Abulrahman, Ibrahim Mohamed, Mwinyi Hajji Mngwali, Abdallah Kheri, Issa Haidari, Abdulaziz Makame/Feisal Salum dk20, Mohamed Issa ‘Banka’, Mudathir Yahya, Ibrahim Hamad ‘Hilika’, Seif Abdallah ‘Karihe’/Khamis Mussa Makamedk56 na Suleiman Kassim ‘Selembe’/Adeyoum Seif Ahmed dk116.
Mapema katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu, Uganda iliichapa Burundi mabao 2-1 hapo hapo Uwanja wa Kenyatta, Machakos.

Haikuwa kazi rahisi kwa The Cranes kumaliza nafasio ya tatu, kwani ililazimika kutoka nyuma baada ya Nahodha wa Burundi, Pierre Kwizera kuanza kuifungia timu yake, kabla ya Saddam Juma Ibrahim kuisawazishia Uganda dakika ya 48 na Issa Dau kufunga la ushindi dakika ya 7

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search