Tuesday, 23 January 2018

AJALI YA BASI YAUA WATU WAWILI
Watu wawili wamefariki dunia na wengine watatu wamejeruhiwa katika ajali ya gari baada ya basi dogo la abiria kampuni ya Mkombozi kugongana uso kwa uso na basi la kampuni ya Walawi katika eneo la Kamanga jijini Mwanza.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza kamishna msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa dereva wa basi la Mkombozi pamoja na abiria mwingine wamepoteza maisha hapo hapo.

"Ni kweli imetokea ajali hiyo na kusababisha vifo vya watu wawili akiwepo dereva la basi dogo la kampuni ya Mkombozi ambaye alifariki hapo hapo baada ya ajali pamoja na abiria mwingine, lakini pia wapo majeruhi watatu ambao wamepelekwa kwa matibabu zaidi" 

Jeshi la polisi linaendelea kufanya uchunguzi kujua chanzo za ajali hiyo.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search