Monday, 15 January 2018

ALIYEWADHALILISHA WATU WEUSI KWA KUTOA MANENO YA KIBAGUZI ATEMWA NA MPENZI WAKE

Aliyewazalilisha Watu Weusi Uingeleza Atemwa na Mpenzi Wake
Kiongozi wa chama cha UKIP nchini Uingereza Henry Bolton anasema kuwa amesitisha uhusiano na mpenzi wake baada ya yeye kuripotiwa kutoa maoni ya ubaguzi wa rangi kumhusu Meghan Markle.

Alisema kuwa mapenzi yao hayataendelea akiwa na wajibu kama kiongozi wa chama lakini hana nia ya kujiuzulu.

Jo Marney alikuwa ametuma ujumbe wa simu kuwa watu weusi wana sura mbaya na mpenzi wake Prince Harry ataichafua familia ya kifalme.

Mataifa ya Afrika yamtaka Trump kuomba msamaha
Bw Bolton alisema kuwa ilikuwa kinyume na katiba ya chama cha UKIP kuonyesha fikra zozote za ubaguzi wa rangi.

Mwanajeshi huyo wa zamani alichukua usukani wa chama cha UKIP kama kiongozi mwezi Septemba, na kuwa kiongozi wa nne katika kipindi cha miaka 18.

Trump asema atamshinda Oprah Winfrey 2020
Bw Bolton 54, alisema kuwa mwanamitindo huyo wa miaka miaka 25 alitimuliwa chamani mara moja baada ya chama kugundua kuhusu maoni yake.

Ujumbe huo ulitumwa wiki tatu baada ya wapenzi hao wawili kuanza uhusiano wao. 

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search