Wednesday, 31 January 2018

AUBAMEYANG AJIUNGA NA ARSENAL

Arsenal have unveiled new signing Pierre-Emerick Aubameyang.
LONDON, UINGEREZA: Uhamisho wa mshambuliaji Pierre- Emerick Aubameyang kutoka Klabu ya Borussia Dortmund kwenda Arsenal umekamilika baada ya mchezaji huyo kusaini mkataba wa miaka mitatu na nusu kwa ada ya Pauni milioni 52.7.
-
Klabu ya Borussia Dortmund imethibitisha uhamisho huo kupitia Mkurugenzi wake wa michezo, Michael Zorc aliyesema anamshukuru mchezaji huyo kwa mafanikio aliyoyaleta Dortmund licha ya matukio yasiyofurahisha yaliyotokea siku za karibuni
-
Aubameyang anafika katika klabu hiyo ya London akiwa katika kiwango cha kutisha cha kupachika magoli, akiwa amefunga magoli 100 katika mechi 119 alizochezea Dortimund kuanzia msimu wa 2015/2016

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search