Friday, 26 January 2018

Breaking News: Aliyekuwa Mkurugenzi wa TBC Tido Mhando Afikishwa Mahakamani

Breaking News: Aliyekuwa Mkurugenzi wa TBC Tido Mhando Afikishwa Mahakamani

Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi.

Mhando anakabiliwa na mashtaka manne ya matumizi mabaya ya madaraka na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh887 milioni akiwa TBC.

Tido alifikishwa mahakamani hapo saa 5:22 asubuhi na aliingizwa katika ukumbi wa mahakama ya wazi kabla ya kusomewa mashitaka hayo matano.

Mhando ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Azam Media anakabiliwa na mashtaka matano ya matumizi mabaya ya madaraka na shtaka moja la kuisababishia TBC hasara ya zaidi ya sh. Milioni 887.

[​IMG]


Mhando alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kati ya mwaka 2006 na 2010. Awali alikuwa Mkuu wa Idara ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la BBC (1999-2006).

Kwa kipindi cha miaka mingi sana alikuwa akifanya kazi ya utangazaji wa radio. alianza Utangazaji mwaka 1969 Radio Tanzania Dar es Salaam, (RTD), baadaye akaenda Kenya, halafu Uingereza na hatimaye akarejea tena RTD inayofahamika kama TBC siku hizi.

Kwa sasa Tido Muhando ni Mkurugenzi Mkuu wa Azam Media.

Tido ameachiwa baada ya kutimiza masharti ya dhamana kwa mashitaka yanayomkabili

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search