Thursday, 25 January 2018

DIVA SASA ATAKA PENZI LA SOUD BROWN

Baada ya Kubwagwa na Heri Muziki Diva Anyapia Penzi la Soudy Brown
Baada ya kubwagana na mpenzi wake Heri Muziki, Diva amefunguka mipango yake ya kuwa na Soudy Brown.

Mtangazaji huyo wa kipindi cha Ala za Roho cha Clouds Fm amesema kwa sasa yupo tayari kubadili dini kwa ajili ya Soudy Brown ambaye ni mtangazaji mwenzake katika kituo hicho.

“Soudy Brown ndio kila kitu kwangu niseme hivyo, urafiki wangu uko karibu kupita kiasi like hakuna kama Soudy I think he my only true love,” Diva ameiambia Bongo5.

“Kwa sababu yeye ni mtoto wa kislam akiniongeza kwenye list nitabadilisha dini na nitaitwa Amina,” amesisitiza.

Hata hivyo ameongeza kuwa tayari anamjua mpenzi wake Soudy Brown ila kitu ambacho watakaa na kujadili. Diva kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Waambie’ ambao amewashirikisha  Mr. Paul na Mwana FA.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search