Tuesday, 9 January 2018

Diwani wa CUF wilayani Ruangwa mjini mkoani Lindi ajiuzulu

Diwani wa CUF anaetambulika kwa jina maarufu Selenge amejivua udiwani diwani huyo alikua hapo hapo Ruangwa mjini kata ya Dodoma miongoni mwa kata mbili za huko mjini Ruangwa.

Ruangwa mjini kuna kata mbili na zote zilichukuliwa na CUF kata moja ipo wazi na sasa CUF amebakiwa na kata moja mjini hapo.

Kuna tetesi za madiwani wawili wa CHADEMA na CUF kata ya matambarare na namichiga wilayani Ruangwa inasemekana nae wapo mbioni kujiuzulu.

Ifahamike ya kua Jimbo hilo ndiyo alilotokea waziri mkuu wa awamu ya tano.

Pamoja na kujiuzulu kwa diwani huyo almaarufu kwa jina la Selenge haijafahamika atatimkia wapi japo kuna tetesi za kutimkia CCM.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search