Wednesday, 31 January 2018

George Weah ameahidi kubadilisha sheria za uraia Liberia

George Weah

Haki miliki ya pichaEPA
Image captionRais mpya wa Liberia ameahidi kukatwa mshahara
Rais wa Liberia George Weah ametoa agizo la kutoa kipengele cha 'kibaguzi' kwenye katiba kinachoruhusu upatakanaji wa uraia kwa watu weusi tu.
Kipengele hicho ni ''baguzi na haifai'' amesema aliyekuwa mwanamichezo nyota wa soka katika hotuba yake ya kwanza ya taifa tangu achaguliwe kuwa Rais.
Aliahidi pia kufuta sheria inayowazuia wenyeji kumiliki ardhi, ikumbukwe kwamba chimbuko la Liberia limetokana na watumwa walioachiwa huru kutoka Marekani mwaka 1847 na kuwa kama bustani ya hifadhi kwa mtu mweusi aliyeachwa huru.
Katiba inamtambulisha mtu mweusi ''Negro'' jina la kibaguzi walilokuwa wakiitwa watu weusi wakati wa utumwa.
Jamii nyingine inayokadiriwa kuwa na watu 4000 ni raia wa Lebanon ambao wameishi nchini Liberia kwa miongo, wananyimwa uraia na haki ya kumiliki ardhi.
Weah anasema vikwazo na vipingamizi vyote hivi viliwekwa wakati ambao havikuwa vinahitajika tena. Mwanasoka huyo wazamani anaongeza kuwa anataka kufutwa kwa kipengele kinacho wanyima raia haki ya kuwa na uraia wa nchi mbili.
''Inakanganya na kupoteza hata maana ya neno Liberia lenyewe ambalo asili yake ni katika lugha ya kilatini likiwa na maana ya Uhuru''
Mwandishi wa habari BBC, Jonatahan Paye Layleh anasema baadhi ya watu katika mji mkuu wa Monrovia wanaona mchakato huu wa mabadiliko ni wa muda mrefu.
Ijapokuwa pia wapo wale ambao wanao hatua yake hii ya kutaka mabadiliko sio kipaombele bali wanataka aweke kipao kwenye kushusha gharama za maisha na si vinginevyo.
Map of Sierra Leone
Bwana Weah ambaye ni mchezaji bora wa Fifa mwaka 1995 na mcheza kandanda wa kwanza kuapishwa kuwa Rais baada ya kushinda kiti hicho kwa kishindo katika uchaguzi mwezi wa Disemba mwaka 2017 baada ya kumbwaga mpinzani wake ambaye alikuwa makamu wa Raisi Joseph Boakai.
Mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea na AC Millan amempokea kijiti, Bi Hellen Sirleaf Rais wa kwanza mwanamke barani Afrika, ambaye aliachia ngazi baada ya kumaliza vipindi vyake viwili vya utawala.
Katika hotuba yake bungeni pia siku ya Jumatatu, Bw Weah alisema atapunguza mshahara wake kwa asilimia 25 kwa sababu serikali na uchumi zimedorora.
''Sarafu yetu inadondoka, mfumuko wa bei unapanda, idadi ya watu wasio na ajira inaongezeka na hazina yetu ya sarafu ya kigeni ni ndogo'' alisitiza Weah na kumuomba waziri mkuu kufuata nyayo zake na kukubali punguzo la mshahara, ''Tukumbuke kwamba tulichaguliwa kuwatumikia wananchi wa Liberia na si kuwatumikisha'' . Wakati wote wa hotuba yake hii Weah alikuwa akishangiliwa.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search