Monday, 29 January 2018

GRACE MUGABE HUENDA AKAKAMATWA NA KUSHTAKIWA

Grace Mugabe Uhenda Akakamatwa na Kushtakiwa

Kauli aliyotoa Rais Emmerson Mnangagwa wiki iliyopita kwamba Grace Mugabe hana kinga ya kushtakiwa imetafsiriwa kuwa huenda mke huyo wa kiongozi wa zamani Robert Mugabe akakamatwa.

Grace alijitengenezea maadui wengi wakati wa utawala wa mumewe ndiyo maana kauli ya Rais Mnangagwa imefungua milango ya kisheria kwa ajili ya kumshtaki mwanamama huyo aliyeogopwa sana Zimbabwe.

Katika mahojiano na Shirika la Habari la BBC alipokuwa kwenye mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) jijini Davos, Uswisi Mnangagwa alisema Grace hana kinga yoyote na anaweza kukamatwa na kushtakiwa mahakamani kwa mashtaka yoyote.

Mwanamitindo wa Afrika Kusini Gabriella Engels ambaye alipigwa na Grace kwa waya wa umeme ameongeza ameanzisha mapambano ya kisheria na anasema amepanga kumshtaki mwanamama huyo.

"Endapo ningepata fursa ya kuona ana rais wa Zimbabwe ningemuomba afanye jambo sahihi nalo ni la kumkabidhi Grace ashtakiwe," Engels aliliambia gazeti la The Standard jana.

Mwanasheria wa Engels inafanya kila liwezekanalo kuhakikisha Grace anapelekwa Afrika Kusini ili aweze kukabiliana na kesi ya kufanya shambulio.

"Tunafahamu kwa sasa hayuko mamlakani kwamba mumewe aliondolewa na kwamba serikali ya Zimbabwe imesema hajawekewa kinga ya kutoshtakiwa,” alisema mama yake  Engels.

"Kutokana na hali ilivyo sasa wanasheria wetu wanashughulikia suala hilo kuhakikisha haki inatendeka kwa mtoto wangu."

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search