Friday, 5 January 2018

HII SASA NI FUNGUA MWAKA -MGANGA WA KIENYEJI AJIUA BAADA YA KUKOSA WATEJA

Wakazi wa eneo la Maili Saba katika Jimbo la Trans Nzoia wamepigwa na butwaa baada ya mganga Joshua Shalongo kujiua kwa sababu ya kukosa wateja na hali ngumu ya maisha.

Shalongo ambaye ni mganga maarufu katika eneo la Kitale nchini Kenya inasemekana suala la kukosa wateja lilimtatiza sana kiasi cha kuchukua uamuzi wa kujiua.

Mwili wake umepatikana ukining’inia kwenye paa la nyumba ukiwa umefungwa kamba taarifa hii imeripotiwa katika jarida la Citizen’s Edaily.

Chief wa eneo hilo Esther Waswa amethibitisha tukio la mganga huyo kujiua.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search