Friday, 19 January 2018

HUYU NDIO KOCHA MPYA WA SIMBA

Club ya wekundu wa Msimbazi Simba leo Alhamisi ya January 18 2018 imetangaza kufanikiwa kumpata mrithi wa kocha Josep Omog aliyefutwa kazi wiki kadhaa zilizopita kwa kushindwa kuuridhisha uongozi katika suala zima la mwenendo wa timu.

Simba Sports Club
Dar es salaam
18/01/2018. TAARIFA KWA UMMA
Klabu ya Simba inayo furaha kubwa kuwajulisha Wanachama na washabiki wake kwamba imempata kocha wake mkuu mpya,Mfaransa Pierre Lechantre.

Kocha huyo mzoefu ataanza kazi mara moja na atasaidiwa na kocha msaidizi wa sasa Masoud Djuma ambae alikuwa akikaimu nafasi hiyo, Kocha Lichantre keshawahi kufundisha vilabu kadhaa duniani kikiwemo kikosi cha Timu ya Taifa ya Cameroun kilichotwaa ubingwa wa Africa 2000.

Kocha huyo pia alipata kuwa kocha bora wa Afrika mwaka 2001 na pia barani Asia mwaka 2012, Lechantre amekuja pia na kocha wa viungo Mmorocco Mohammed Aymen Hbibi

Leo jioni kocha Lechantre ataishuhudia Simba ikicheza na Singida United kwenye Uwanja wa Taifa.

IMETOLEWA NA
HAJI S MANARA

MKUU WA HABARI SIMBA SC

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search