Wednesday, 10 January 2018

Huyu ndio mchezaji soka mwenye pesa chafu kuwazidi Ronaldo, Messi


Je unaweza kufahamu ni mchezaji gani wa soka ambaye ni tajiri zaidi duniani? Watupie mbali Cristiano Ronaldo na Lionel Messi bila ya kumsahau Coutinho na Neymar ambaye ni mchezaji anayeshikilia rekodi ya kusajiliwa kwa kiasi kikubwa cha fedha duniani na PSG huyu ni kinda wa miaka 19 anayecheza soka Uingereza.

Umeshamfahamu mchezaji huyo ni nani? Faiq Bolkiah mwenye umri wa miaka 19 ambaye yupo kwenye klabu ya Leicester city ndio mwanasoka tajiri zaidi. Hutaki kuamini?

Kijana huyu ni ndugu wa Sultani Hassanal Bolkiah wa taifa la Brunei linalozungukwa na Malaysia na Bahari ya Kusini ya China. Faiq ana utajiri wa kiasi cha dola bilioni 20 ambapo ni zaidi ya mara 20 ya utajiri wa P Diddy na ni zaidi ya mara 21 ya utajiri wa Jay Z.

Winga huyu wa wa klabu ya soka ya Leicester alianza kucheza soka katika klabu ya AFC Newbury ya Uingereza. Mwaka 2009 Southampton walimuongeza mchezaji huyo katika academy yao hata hivyo hakuweza kupewa mkataba.

Faiq pia amewahi kuichezea timu ya vijana ya Arsenal kwa mwaka mmoja na baadae alifanikiwa kupata ofa katika timu ya vijana ya Chelsea na kusaini mkataba wa miaka miwili lakini Bolkiah aliondoka klabuni hapo baada ya mwaka mmoja na kujiunga na klabu ya soka ya Leicester kwa muda wa miaka mitatu.

Utajiri wa Faiq haujapatikana katika soka kutokana na muda wake na bado hajafikia kiwango cha kupokea mzigo mzito kwa wiki kama ilivyo kwa Ronaldo, Messi, Pogba, Neymar, Oscar wa Shanghai SIPG na wengine. Chanzo cha utajiri wa Bolkiah ni baba yake aitwaye Jefri Bolkiah ambaye ni kaka yake na Sultani wa Brunei.

Jefri ameripotiwa kutumia zaidi ya pauni bilioni 10 kwa miaka 15 kama mkuu wa shirika la uwekezaji wa Brunei na inasemekana kwamba mzee huyo huyo anamiliki magari zaidi ya 2,300 yakiwemo magari ya kifahari kama Bentleys, Ferrari na Rolls Royces.

Katika tukio jingine ambalo liliwahi kuwashtua watu wengi ni pale mzee Jefri aliposherehekea siku yake ya kuzuliwa ya kutimiza miaka 50 kwa kufanya tamasha binasfi na alimualika marehemu Michael Jackson kwa ajili ya kutumbuiza pamoja na kujenga uwanja wote wa tamasha hilo na kumlipa msanii huyo kiasi cha paundi milioni 12.5.

Lazima utakuwa unajiuliza ni kwanini Faiq Bolkiah anacheza mpira licha ya kuwa na utajiri huo mkubwa, winga huyo wa Leicester City aliwahi kusema hivi wakati alipohojiwa, “I’ve played football since as early as i can remember and from a young age. I’ve always enjoyed going out on the field and having the ball at my feet.”

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search