Monday, 29 January 2018

Jafo Atoa Agizo Hili kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri

 JafoAtoa Agizo Hili kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri (DED)

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Selemani Jafo amewaagiza wakuu wa wilaya na wakurugenzi watendaji wa halmashauri (DED) kutunza siri za Serikali.

Jafo ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Januari 29,2018 mjini Dodoma alipofungua mafunzo ya uongozi kwa wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa mikoa sita.

Mafunzo hayo ni mwendelezo wa ambayo yanatolewa kwa viongozi wa kada hiyo.

Waziri Jafo amesema ujenzi wa Serikali utakuwa mzuri iwapo viongozi hao watakuwa makini na kutunza siri.

"Hivi unakuwaje wewe mkurugenzi au mkuu wa wilaya unapeleka siri za Serikali kwenye mitandao ya kijamii na nyingi unaziona kwenye WhatsApp, inatia aibu sana," amesema Jafo.

Amewataka wakurugenzi kujipambanua na kusimamia miradi ya maendeleo katika kukusanya mapato na kuyatumia vyema na hasa ya ndani.

Jafo amesema tatizo kubwa kwa wakurugenzi ni kutofanya uamuzi kwa haraka 

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search