Tuesday, 23 January 2018

Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma awaonya viongozi wa Serikali na wanasiasa kuacha kuingilia muhimili wa Mahakama

[​IMG]

Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, amewaonya viongozi wa serikali na wanasiasa, kuacha kuingilia mhimili wa Mahakama na kuvunja amri zake.

Jaji Juma ametoa onyo hilo leo Januari 23, 2018 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya wiki ya sheria yatakayofikia kilele, Februari Mosi mwaka huu.

Amesema kwa mujibu wa Katiba ya nchi mamlaka ya utoaji wa haki ni ya mahakama tu, kutoa wito kwa mahakama kuchukua hatua kwa wale wote wanaokiuka amri za mahakama.

"Nawakumbusha wananchi na viongozi mbalimbali nje ya mahakama kuwa kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, mamlaka za kikatiba na kisheria wabaki ndani ya maeneo yao ya kikatiba na wajiepushe na kuingilia maeneo yaliyo ndani ya haki, hadhi na mamlaka ya kikatiba ya mahakama".

Kuhusu maadhimisho ya wiki ya sheria, amesema yatafanyika katika viwanja vya Mnanzi Mmoja na kuzinduliwa Januari 27 na Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete.

Amesema siku ya kilele cha maadhimisho ya wiki hiyo, mgeni rasmi atakuwa Rais John Magufuli.

Chanzo: Mwananchi

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search