Wednesday, 24 January 2018

JAJI MSTAAFU ROBERT KISANGA AFARIKI DUNIA

Rais wa Chama cha Majaji Wastaafu, Thomas Mihayo akizungumza na MCL Digital leo Jumatano Januari 24,2018 amesema Jaji Kisanga alifariki dunia jana jioni.

Jaji Mihayo amesema Kisanga alifariki dunia akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Regency jijini Dar es Salaam.

Amesema taarifa zaidi zitatolewa baadaye.

Mbali ya shughuli za Mahakama, Jaji Kisanga alikuwa mwenyekiti wa kwanza wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search