Thursday, 11 January 2018

JAMAA ACHOMA NYUMBA AKIUA BUIBUI

Buibui huyo anaaminika kuwa buibui mkubwa aina ya 'wolf spider'

Mwanaume mmoja katika mji wa Redding kaskazini mwa California, Marekani anadaiwa kuchoma moto nyumba akijaribu kumuua buibui.

Kisa hicho kilitokea Jumapili kwa mujibu wa vyombo vya habari Marekani.

Mmoja wa walioshuhudia, ambaye alikuwa anaishi katika nyumba hiyo kubwa ya makazi, ameambia gazeti moja California kwamba buibui huyo huenda alichangia kueneza moto huo chumbani, akikimbia akiwa anaungua.

Haijabanika iwapo buibui huyo alinusurika.

Hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa, lakini wakazi wa jumba hilo waliondolewa.

Afisa wa idara ya wazimamoto eneo hilo Gerry Gray ameambia BBC ni kwenye kwamba moto ulizuka katika jumba hilo lakini akasema chanzo cha moto huo bado kinachunguzwa.

"Taarifa kuhusu 'buibui' zilitolewa na raia walioshuhudia, waliokuwa eneo la mkasa, na bila shaka zinatumiwa katika uchunguzi.

Buibui huyo alikuwa aina ya 'wolf spider' ambao ni buibui wakubwa.

Idara ya kuzima moto imeambia gazeti la Redding Record Searchlight kwamba dalili zinaonesha moto huo uliwashwa kwa mwenye.

Redding, eneo ambalo kisa hicho kilitokea, ni mji ulio maili 162 (261km) kaskazini Sacramento.

Walioshuhudia wanasema buibui huyo alieneza moto alipokimbia na kujificha kwenye mto.

Mto huo ulishika moto na moto huo, na ingawa wakazi waliweza kuuzima hapo, ulikuwa tayari umeenea maeneo mengine ya jumba hilo.

Maafisa wanasema moto huo ulisababisha uharibifu wa takriban $11,000 (£8,000) na baadhi ya vyumba vya jumba hilo vitahitaji kukarabatiwa kabla ya watu kuishi huko tena.
Chanzo-BBC

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search