Thursday, 25 January 2018

JINSI YA KUPANGILIA MLO WAKO UKITAKA KUPUNGUZA MWILI.

Ili kupunguza uzito cha kwanza kuzingatia ni kuweka nia.
Baada ya kuweka nia ya kutaka kupunguza uzito pangilia mlo wako wa kila siku na ratiba zako zingine kama kufanya mazoezi n.k.

Na hapa utapata kuelewa mpangilio wa vyakula unavyotakiwa kuvitumia katika mlo wako wa kila siku kuanzia asubuhi mpaka jioni.


ASUBUHI.
Hapa asubuhi unapooamka kupata kifungua kinywa unatakiwa kutumia vyakula ambavyo vitajaza tumbo lako na kukufanya kujihisi umeshiba na kukaa muda mrefu bila kupata hamu ya kula.
Hii inakusaidia kupunguza hamu ya mara kwa mara ya kula kula au unapotembea njiani kutamani vitu vidogovidogo ili kuufanya mwili utumie mafuta yaliyoifadhiwa mwilini mbadala wa chakula utachakula.

MCHANA.
Kwa kutegemea na chakula ulichokula asubuhi kinaweza kukufanya uvuke mchana kutwa bila kujihisi njaa na kama utahitaji kula wakati huo ni vizuri ukaangalia matunda ambayo unaweza kula kidogo tu na kujaza tumbo mfano Ndizi, na vyakula vingine kama hivyo .


JIONI.
Jioni na wakati wa kwenda kulala hapa tumia chakula kidogo na vyakula ambavyo vinachochea uyeyushaji wa mafuta mwilini. Kwa kutumia vyakula hivyo vitachochea mwili wako na kuwa na uhitaji mkubwa wa nishati ili kufanya shughuli zake hivyo mwili utayeyusha mafuta na kuyatumia kama nishati mwilini.

Hivi ni baadhi ya vyakula ambavyo vitakusaidia kuweza kupunguza kiwango cha chakula unachokula kwa siku na vyakula ambavyo vinachochea uyeyushaji wa mafuta mwilini.


1. Tufaha (Apple)

Tunda hili lina kirutubisho kinachoitwa Pectin kazi yake kubwa ni kupunguza kasi ya umeng’enywaji wa chakula na kukufanya ujihisi umeshiba na kukaa muda mrefu bila kula.
Kula na maganda yake ni vizuri Zaidi kuliko kulimenya.   

2. Ndizi

Ni ndizi mbivu hasa zile ambazo bado hazijaiva vizuri zikiwa bado zina ukijani kijani. Ndizi hizo zina starch nyingi ambayo umeng’enywa taratibu sana kwenye mfumo wa chakula na kukaa tumboni kwa muda mrefu, hivyo kukufanya kukaa muda mrefu bila kula.


3. Kabichi.

Kabichi ina kalori ndogo pia ni chakula cha kukufanya kokosa hamu ya kula kwa kuwa inakaa tumboni muda mrefu.4. Karoti.

Karoti pia zina nyuzi lishe na maji ya kutosha. Ukaa tumboni kwa muda mrefu na kukufanya kukosa hamu ya kula kula ovyo. Ni muhimu kuzipika karoti, kwani tafiti zinaonesha kuwa karoti zilizopikwa zianakuwa na viondoa sumu vingi mara tatu Zaidi ya karoti ambazo hazijapikwa.


5. Pilipili.
Pilipili hizi zina kampaundi inayoitwa Capsaicin ambayo huchochea uyeyushaji wa mafuta mwilini kutumika katika matumizi mbalimbali ya mwili.


6. Kahawa.
Kafeini kwenye kahawa inachochea uyeyushaji wa mafuta mwilini. Ila kuwa makini na kiwango cha sukari utakayoweka kwenye kinywaji chako.


7. Limao.

Kukamulia malimao katika kinywaji au chakula ni njia nzuri ya kuongeza ladha katika chakula chako wakati ukiwa katika nia ya kupunguza uzito.8. Machungwa.
Machungwa kama malimao yana kiwango kidogo cha kalori vilevile yana nyuzi lishe za nyingi ambzo zitakusaidia kuondoa hamu ya kulakula ovyo.


9. Viazi.

Aina zote za viazi, viazi mviringo na viazi vitamu vyote vina aina ya starch kama ya ndizi mbivu ambayo umeng’nywaji wake kwenye mfumo wa chakula ni wa taratibu sana. Navyo hukufanya kukaa muda mrefu bila kuhisi hamu ya kula.10. Maboga.

Maboga pia yana wingi wa nyuzi lishe. Ukiwa katika mpango wa kupunguza uzito vyakula hivi ni vya kuzingatia katika mlo wako wa kila siku.


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search