Friday, 12 January 2018

KIJANA AUCHAPA USINGIZI BILA WASIWASI PEMBENI YA RELI

Image may contain: one or more people, bridge, outdoor and nature

Kijana mmoja maarufu kwa jina la Sharobaro mjini hapa Mororgoro, aliyekadiriwa kuwa na umri wa miaka 20, ameuchapa usingizi chini ya daraja la reli kisha kupoteza maisha baada ya kukatwa vipande viwili na treni.
Tukio hilo ambalo Ijumaa Wikienda lilifika punde baada ya kujiri, lilitokea kwenye daraja lililopo Barabara ya lringa- Morogoro, eneo la Msamvu, mchana wa Ijumaa iliyopita na kuibua masikitiko makubwa.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, wasamaria wema waliishuhudia maiti ya kijana huyo ikiwa imekatwa vipande viwili ndipo wakatoa taarifa kwa uongozi wa serikali ya mtaa huo ambao nao ulitoa taarifa polisi.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search