Wednesday, 10 January 2018

Korea Kaskazini na Kusini Kufanya Mazungumzo ya Kijeshi

Korea Kaskazini na Kusini Kufanya Mazungumzo ya Kijeshi
Korea Kaskazini na Kusini zimekubaliana kufanya mazungumzo ya kijeshi ili kuondoa wasiwasi uliopo mipakani baada ya mkutano wa kwanza katika kipindi cha miaka miwili.

Korea Kaskazini pia itatuma ujumbe katika michezo hiyo ya msimu wa baridi itakayofanyika Korea Kusini mnamo mwezi Februari.

Makubaliano yaliafikiwa kurudisha nambari ya simu ya jeshi ilioondolewa mwaka mmoja uliopita , kulingana na serikali ya Korea Kusini.


Hatahivyo ujumbe wa Korea Kaskazini ulipinga ajenda ya kusitisha mpango wa kinyuklia , Korea Kusini iliongezea.

Wanajeshi wa Korea Kusini wakipiga doria katika mpaka wao na Korea Kaskazini
Idara ya maswala ya kigeni ilisema kuwa Marekani inaendelea na majadiliano na maafisa wa Korea Kusini ambao watahakikisha kuwa kishiriki kwa Korea Kaskazini katika michezo ya Olimpiki hakutakiuka kivyovyote vikwazo vya Umoja wa mataifa.

Baada ya siku moja ya mazungumzo , pande zote mbili zilitoa taarifa ya pamoja ambayo ilithibitisha kuwa wamekubaliana kufanya mazungumzo ya kijeshi ya kuondoa wasiwasi uliopo.

Korea Kaskazini pia ilikubali kutuma kikosi cha michezo ya Olimpiki ikiwemo, wanariadha, mashabiki, wawakilishi wa sanaa, na kikosi cha kuonyesha mchezo wa Takweondo mbali na vyombo vya habari katika michezo hiyo huku Korea Kusini ikikubali kutoa vifaa na huduma zote za kikosi hicho.

Taarifa hiyo pia ilizungumzo kuhusu mabadilishano ya mawazo mbali na mazungumzo ya ngazi za juu kuhusu kuimarisha uhusiano wa mataifa hayo mawili kulingana na chombo cha habari cha Korea Kusini cha Yonhap.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search