Wednesday, 31 January 2018

Kuolewa Mke wa Pili si Dhambi- Tausi Mdegela

Kuolewa Mke wa Pili si Dhambi- Tausi Mdegela
KOMEDIANI matata wa Bongo Movies, Tausi Mdegela amefunguka kuwa, ikitokea akapata mwanaume wa kumuoa, hata kama ana mke haina shida kuolewa mke mwenza au wa pili kwani kama ni Muislam, dini inaruhusu.


Tausi alifunguka hayo juzikati baada ya kuzagaa kwa habari kwamba anatarajia kuolewa na mwanamuziki wa Taarab, Prince Amigo na kueleza kuwa, siyo kweli, bali ilikuwa ni kava la wimbo wake, lakini ikitokea amepata mwanaume, yupo tayari kuolewa mke wa pili.

“Kuolewa mke wa pili siyo dhambi, ikitokea nimepata wa kunioa, hata kama ni mke wa pili, sioni shida ilimradi awe Muislam kwa kuwa dini inamruhusu,” alisema Tausi.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search