Tuesday, 9 January 2018

Kutoka Checkpoint, Pugu: Aliyekuwa mgombea Ubunge jimbo la Ilala 2015 kupitia CHADEMA, Muslim Hassanali ajiunga na CCMUtambulisho wa watu walioudhuria;
  • Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Wilaya
  • Wajumbe wa sekretarieti ya Chama wilaya ya Ilala
  • Madiwani tofauti tofauti
  • Mbunge wa Jimbo la Segerea
  • Viongozi wa Mkoa pia wapo
Mgeni rasmi ni kwenye mkutano huu ni Makamu mwenyekiti wa CCM Bara, Mzee Mangula.

Polepole anaongea na kusema;
Aliye hamia CCM kutoka CHADEMA ni Muslim Hassanali, aliyegombea ubunge wa jimbo la Ilala 2015 kwa tiketi ya CHADEMA ambaye pia ni mjumbe bodi ya wadhamini wa chama hicho

1.jpg
Pichani: Muslim Hassanali​

Baada ya kutambulishwa na Humphrey Polepole anavaa shati la kijani na kofia ya CCM, na hapa anakula kiapo cha kuitumikia CCM

kiapo.jpg ​

Muslim Hassanali anaongea baada ya kula kiapo;
Mtu alitoka upinzani kwenda CCM anahesabika eti amehongwa, mimi si wa kanda ya ziwa na sijahongwa mimi ni kijana wa Dar na mzalendo wa nchi hii.

Haikuwa kazi rahisi kuchukua maamuzi ya kuihama CHADEMA na kujiunga CCM, Ila imebidi niweke maslahi yangu binafsi pembeni na kujiunga CCM ili nipambanie nchi yangu

Kwa muda wa mwaka mmoja nimijitafakari sana na sasa nimmeamua kumuunga mkono mhe. Magufuli kwa kupigania nchi yangu. Kuna vitu tulikuwa tunapigia kelele na CHADEMA kama mikataba ya madini ambapo leo sina haja ya kupiga kelele kutokana na anayoyafanya rais na Serikali. Pia na utumiaji mbaya wa madaraka lakini kwa utawala huu wa Magufuli watu wanapata imani

Nimekosoa Serikali vya kutosha ila sasa ni muda wa kushirikiana nayo, sio wakati wa kuikosoa serikali na kuichafulia jina

Sijawahi kuwa mwana CCM tangu nimezaliwa lakini leo najisikia faraja kujiunga na kundi kubwa na wanachama wa CCM

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search