Tuesday, 2 January 2018

LOWASSA ATOA KAULI YA MWAKA MPYA...UJUMBE UNAHUSU WATANZANIA WOTE

Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati kuu CHADEMA, Mh. Edward Lowassa amewataka watanzani kwa ujumla wao wote wakatae kugawanywa kwa sababu yoyote ile.

Mh. Lowassa ametoa ujumbe huo kupitia mtandao wake wa kijamii wakati akitoa salamu za Mwaka Mpya 2018.

Mh. Lowassa ameandika "Tunapouanza mwaka huu mpya niwaombe watanzania wenzangu tukatae kugawanywa kwa sababu yoyote ile. Umoja na mshikamano ndio nguzo yetu. Nawatakia Heri na Fanaka ya mwaka mpya 2018".

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search