Wednesday, 10 January 2018

Maandalizi AFCON U17 yazidi kushika kasi

Shirikisho la soka nchini TFF limeendelea na maandalizi ya kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 (Serengeti Boys) itakayoshiriki fainali za AFCON U17 zitakazofanyika hapa Tanzania.

Taarifa ya TFF leo imeeleza kuwa vijana 43 leo wameanza kambi ya wiki mbiili kwenye uwanja wa Karume uliopo Makao makuu ya TFF Ilala jijini Dar es salaam na itamalizika Januari 21 mwaka huu.

Kambi hiyo ni sehemu ya maandalizi ya timu hiyo ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17 kuelekea fainali hizo za soka la vijana barani Afrika.

Tanzania itashiriki michuano hiyo bila kupita katika hatua ya mchujo kutokana na faida ya kuwa mwenyeji. Mei 28 mwaka 2017 nchini Mali, Rais wa Shirikisho la soka barani Afrika Ahmed Ahmed alikabidhi bendera ya CAF kwa viongozi wa TFF kama ishara ya kuwa mwenyeji.

Fainali za mwaka 2017 Serengeti Boys ilishika nafasi ya tatu katika fainali zilizofanyika nchini Gabon. Moja ya wachezaji waliokuwepo kwenye kikosi hicho ni mshambuliaji wa Yanga Yohana Mkomola na golikipa Ramadhani Kabwili.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search