Friday, 26 January 2018

Mashabiki Wamshauri Snura Kuachana na Singeli

Mashabiki Wamshauri Snura Kuachana na Singeli


Siku chache tangu aachie ngoma mpya ya Moyo Niache akimshirikisha Dogo Aslay, msanii Snura Mushi amesema amepata maoni kutoka kwa mashabiki wengi wakimtaka aachane na muziki wa kisingeli.

Snura akizungumza na MCL Digital, amesema wimbo huo wa taratibu ni wa kwanza kuuachia tangu aingie katika fani ya muziki, umepokewa vizuri na mashabiki ambao wamemshauri aendelee na staili hiyo.

Akimzungumzia Dogo Aslay ambaye ni kati ya wasanii wanaofanya vyema katika muziki wa Bongo Fleva, Snura amesema hakupata wakati mgumu kumpata ili kufanya naye kazi.

“Ni kweli baadhi wamekuwa wakilalama kuhusu ugumu wa kumpata Aslay kufanya naye kazi, lakini namshukuru Mungu kazi zangu kufanya vizuri kumenisaidia kumpata kirahisi,” amesema.

Snura ambaye jina lake lilianza kujizolea umaarufu kupitia filamu, tangu aingie kwenye muziki ameshaachia vibao kama vile Najidabua, Chura, Zungusha, Majanga na Shindu. 

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search