Wednesday, 24 January 2018

Mchungaji Msigwa afikishwa mahakamani Hila za polisi za kuzuia dhamana zatupiliwa mbali

Image result
CHINI YA ULINZI: Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa (CHADEMA) na wenzake 12 wamefikishwa ktk Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa kwa tuhuma za kuchoma nyumba ya Katibu wa UVCCM mkoani humo na kubomoa nyumba ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwangata aliyehamia CCM, Angelus Lijuja.

Hatimaye Rev.Msigwa na viongozi wengine 13 wamepandishwa kizimbani leo katika Mahakama ya Iringa , polisi walijaribu kama kawaida yao kuzuia dhamana zao kwa kiapo cha RCO lakini Mahakama imetupilia mbali kiapo hicho na imewapatia dhamana .

Wameshitakiwa kwa makosa yanayoitwa eti kula njama za kuharibu mali na kuvunja na kuchoma nyumba ya kada wa UVCCM Moto , Haya yana mwisho.

=====

Mh Peter Msigwa na Viongozi 12 Wa Chadema Wapata DHAMANA Mahakamani*


Waliofikishwa Mahakamani ni:-

1. Peter Msigwa
2. Leonce Marto
3. Samwel Nyanda
4. Adrey George Mkemwa
5. Rehema Mbetwa
6. Maneno Rashid Mbuma
7. Rody Jumanne Makimwa
8. Deogratius Faustine Kisumi
9. Patrick Madat
10 Luioniso Kadaga.
11. Gama Msigwa

Walifikishwa Mahakamani kwa
*Makosa*
1. Kula njama kutenda kosa la kuleta madhara kwenye mali.

2. Uharibifu wa mali. Kati ya tarehe 15/1/2018 waliharibu nyumba ya Anjelus Lijuja yenye thamani ya million saba.

*KIAPO CHA MPELELEZI WA MKOA*

Mwendesha mashtaka ameleta ombi kwamba washtakiwa wasipewe dhamana kwa kulinda usalama wao. Wabakie ndani hadi hapo upelelezi utakapokua umekamilika. (sect. 48 mwenendo wa dhamana)

Wakili: hatujapokea hicho kiapo na hatujui kilichopo ndani. Ifahamike suala la dhamana ni haki ya mtuhumiwa na siyo priviledge. Its a right. Madhumuni yake yako wazi kutokana na kanuni ya presumption of innocent. Watuhumiwa bado hawajahukumiwa kutenda kosa. (Reference of other reported cases to support the defence)

Mahakama imetupilia Mbali Kiapo hicho na kutoa dhamana kwa watuhumiwa

Hata Jeshi La Police Mkoa Iringa Bado linamshikilia Mwenyekiti wa Bavicha wilaya kilolo Mwalimu Kuzen Msungu na Limeshindwa kumfikisha mahakamani pamoja na watuhumiwa Wezake,

Tunatoa wito kwa jeshi la Polisi Kama linaona hakuna sababu ya kupeleka mahakamani Kamanda Msungu Limwachie

Tunatoa Pongezi kwa Viongozi,wanachama ,na wafuasi wa chadema kwa kuonesha ushirikiano,Umoja na Mshikamano

_imetolewa na_

*JACKSON MNYAWAMI*
*KATIBU WA BAVICHA*
*MKOA WA IRINGA.*

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search