Thursday, 11 January 2018

MJUE NDULI IDDI AMINI DADA - MTOTO WA SANGOMA ALIYETIKISA DUNIA


1. Mzaliwa wa Mwaka 1925 huko Kokobo Magharibi ya Jimbo la Mto Nile, Idd Amin Dada ni Rais wa tatu wa Uganda na yumkini Rais Pekee ambaye hakuna kumbukumbu zozote za shule aliyosoma kwani baada ya baba yake kuitelekeza familia yao, alilelewa na mama yake aliyekua 'mpigaramli' ama sangoma na ambaye hakuhangaika kumpeleka shule kwani muda mwingi alikua kwenye 'kamati ya ufundi'. Hii pia inatokana na ukweli kwamba hakuna popote alipowahi kuandika wala kuruhusu mtu yoyote kuandika juu ya historia ya maisha yake.
2. Nduli Amin alioa jumla ya Wake 6 na kupata watoto 40!! mmoja ya wakeze alikutwa amechinjwa kinyama baada ya kubainika amechepuka na kuzaa nje ya ndoa. Fashisti Iddi Amini alikua analala na wake wawili kwenye kitanda kimoja kwa zamu (picha zipo).
3. Licha ya 'kutoenda shule' Amini alijiunga na Jeshi la Kikoloni la Mfalme (KAR) kama mpishi na kupanda hadi cheo cha juu kabisa cha Luteni ambacho ni Waafrika wawili tu walikifikia akiwemo yeye na Milton Obote Rais wa Kwanza wa Uganda.
Ikumbukwe hili lilikua jeshi la wazungu na Amin alipanda cheo kutokana na kupendwa sana na wazungu kwa kuwa alikua na vipaji vingi sana na hasa Ndondi.
4. Alijichagua na kujiapisha kuwa Rais wa Uganda baada ya Mapinduzi ya Kijeshi yaliyomuondoa Milton Obote mwaka 1971 na kuongoza kwa miaka nane hadi 1979.
5. Aliua zaidi ya Waganda LAKI TATU kwa kipindi cha miaka nane aliyodumu madarakani kabla ya kusambaratishwa na majeshi ya Tanzania mwaka 1979.
Yasemekana Nduli Amin alikua akitafuna nyama za watu aliowaua kwa mkono wake mwenyewe huku vichwa vingine akiviweka kwenye jokofu.
Japo inasemekana ni kwa imani za kishirikina na kwa kuwa huyu bwana alikuwa mchawi na mganga kutoka kwa mama yake......
Japo inasemekana ni kwa imani za kishirikina na maagizo toka 'kamati yake ya ufundi'.
6. Aliwahi Kuwatimua Raia wote wenye asili ya India na Pakistani mnamo mwaka 1972 akitaarifukwamba alitumiwa ujumbe na Mungu' akiwa ndotoni na kutaifisha mali zao zote. Yasemekana jumla yao wanaweza kufika kati ya 40000 hadi 80000.
7. Alijipa vyeo kibao ikiwemo cha Field Marshal, AL HAJ, Doctor nk na ili kutimiza ndoto yake ya kuwa na vyeo vyote duniani na hasa cha Mfalme kamili, yasemekana alituma barua ya posa kwa Malikia Elizabeth II ili akamilisha vyeo vyote duniani kikiwamo cha UFALME-KING....
8. Aliwahi kuwa Bingwa wa Ndondi za uzito wa Juu nchini Uganda na alishika rekodi hiyo kwa miaka tisa kati ya 1951 hadi 1960.
Licha ya historia ya maisha ya ukatili na udhalimu wa kutisha, Iddi Amini hajawahi kukamatwa wala kufikishwa kwenye mahakama yoyote hadi umauti wake katika Hospitali ya King Faisal Jedah mnamo mwaka 2003 nchini Saudi Arabia alikokua akiishi uhamishoni baada ya kuugua kwa muda mrefu.
10 Ingawa WAGANDA walisheherekea wakati Iddi Amini anaingia Madarakani, hao hao walisherehekea baada ya Amin kusambaratishwa na majeshi ya Tanzania kutokana na kumchoka kwa jinsi alivyotawala nchi kama nyumbani kwake na kupendwa kuabudiwa kama 'mungu mtu'
11. Funzo kuu aliloacha Iddi Amini mwishoni mwa uhai wake ni pale alipoacha wosia mzito kwamba mikono yake iwe inaonekana nje ya jeneza akimaanisha kwamba alikuja duniani hana kitu na anaondoka akiwa hana kitu na yote aliyoyafanya yamekuwa ubatili na kujilisha upepo ....nukuu ambayo imedukuliwa na watu kadha mashuhuri duniani.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search