Wednesday, 10 January 2018

Mkutano wa Magufuli na Lowassa Ikulu: Waliofaidika na Waliopoteza

Sote tunafahamu siku ya tarehe 9, January 2018 rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania alimualika na kukutana na kisha kujadili mambo kadhaa na ndugu Lowasa pale kwenye nyumba ya Taifa. Japo mpaka sasa sote hatufahamu ni kitu gani wawili hao waliongea lakini tunaweza kujadili maelezo aliyoyatoa kila mmoja wao mara baada ya kumaliza kikao chao. 

Sote tunajua historia ya ndugu Lowasa katika nchi hii, akiwa mwana CCM kisha mtuhumiwa wa kashfa za ufisadi, baadae moja kati wanaoweza kugombea nafasi ya urais kupitia CCM na kisha kuwa mgombea urais CHADEMA/UKAWA. Kilichofuata baada ya hapo ni stori anayoifahamu kila mtu. 

Kutokana na wawili hao kukaa pamoja na kisha kutoa maoni yao kuhusu kila mmoja (counterpart) , naona kuna watu watafaidika na wengine watapata hasara(kisiasa). Embu tutazame jambo hili:-

1. JPM na CCM 

*Wameweza kupata sifa ya kile wanachofanya sasa nchini. Wakati kuna kundi kubwa la Watanzania likilalamikia hali ya uchumi, demokrasia na haki za binadamu nchini, kuna kundi lingine kubwa ambalo limekuwa likisifia kile anachofanya JPM na serikali yake. Lowasa amekuja kuongeza nguvu kwenye kundi la pili na nguvu imekuwa kubwa kwakuwa wengi wa wanamuunga mkono Lowasa wapo kwenye la kwanza. 

*JPM na CCM wamepoteza moja kati ya hoja ya msingi kuhusu Lowasa na CHADEMA ni kundi la mafisadi. Miaka yote tangu mwishoni mwa mwaka 2015 hii hoja CCM waliipokea kutoka CHADEMA na sasa kuna hati hati walioiazima hoja wakairudisha kwa wenye hoja. Lowasa akirudi CCM hii hoja haitaongewa tena, lakini hata asiporudi JPM alishafunga hii hoja pale jana aliposema MZEE LOWASA AMEIFANYIA HII NCHI MAKUBWA.

*CHADEMA wamepoteza sehemu flani hususani kwenye uzito wa hoja yao ya JPM na CCM wanafanya vibaya kwenye uchumi, siasa na huduma za kijamii. Hii ni kwasababu mgombea wake wa urais 2015 amesema JPM anafanya vizuri. Sisemi maneno ya Lowasa yanabadilisha ukweli ki uhalisia, ila yanabadilisha mwenendo wa ukweli kisiasa/kipropaganda. 

*CHADEMA wamefaidika kwenye hoja ya kwamba wao ni chama kinachokumbatia mafisadi. Kwanza wamepata fursa ya kuachana na Lowasa kwa kitendo alichokifanya akijua wazi maoni aliyotoa ni kinyume na msimamo wa chama lakini pia alifanya pasipo achilia mbali kupewa ruhusa bali hata kukitaarifu chama chake kuhusu mkutano wake na JPM. Ikumbukwe yeye sio mwanasiasa binafsi. 

Kwa kutambua kwamba baadhi ya wana CHADEMA hawapendi uwepo wa Lowasa kwenye chama, kumuondoa Lowasa hususani kwa hili lililojitokeza itakuwa ni karata yao dume.

Hapa pia kama JPM amemsifia Lowasa basi CHADEMA watakuwa kifua mbele kwamba mlisema tupo na Lowasa fisadi, mbona mkuu wenu amesifia na kupongeza Mchango wake kwenye Taifa hili. 

Mnyika na wana CHADEMA ambao hawakubali uwepo wa Lowasa chamani wame prove walikuwa, na mpaka sasa wapo right. Pengine hata wale waliopo nje ya CHADEMA kwasasa kutokana na ujio wa Lowasa chamani kama Dr. Slaa wamedhihirisha kwamba walikuwa sawa huko nyuma. 

Mbowe na wana CHADEMA waliomualika Lowasa wamedhihirisha kwamba maamuzi yao yalipaswa kuhojiwa wakati ule, na yanapaswa kuhojiwa sasa. 

Lowasa amepata moja kati ya vitu muhimu sana kwenye maisha yake. Kwasasa ni ngumu sana kuja kusikia kutoka CCM ama CHADEMA kwamba yeye ni fisadi. CHADEMA walimsafisha 2015, CCM walimsafisha kabla na dalili za kumsafisha sasa zimeanza, kupitia kauli za Mkuu wa kaya ambaye ndio mwenyekiti wa chama. 

Lowasa amepoteza moja kati ya ndoto za maisha yake. NDOTO YA KUGOMBEA NA KUWA RAIS. Kama alikuwa ana nafasi hiyo kupitia CHADEMA mwaka 2020 kwa asilimia hata 20, kwasasa atakuwa na asilimia sifuri. Kiufupi jana ndio amefuta any possibility ya yeye kugombea urais mwaka 2020 kupitia CHADEMA. Kugombea kupitia CCM ndio asahau kabisa. 

Dr. Slaa na wana CHADEMA walihamia CCM kwa hoja ya CHADEMA kupokea mafisadi itabidi na wao wabadili gia angani kwani dalili zinaonesha Lowasa moja kati ya reference ya ufisadi kwa mujibu wao anaenda kuwa karibu na wao kuliko alivyo karibu na CHADEMA. 

Wanasiasa wamepoteza. Wanasiasa (wengi wao) wamedhihirisha kwamba wao ni wanafiki. Mfano kitendo cha fisadi Lowasa (alivyoitwa mwanzo), jana kuitwa waziri mkuu mstaafu (neno ambalo mwanzo hawakutaka kabisa kulitumia). Mfano kuonekana adui wa Taifa na mahakama za mafisadi kuundwa, leo anaonekana yeye kuwa kati ya viongozi wa kukumbukwa kwenye Taifa hili kutokana na michango yao. Kutoka kuwa anaharibu uchumi leo kuwa anafanya vizuri kwenye uchumi. Hitimisho hapa ni kwamba wanasiasa wengi ni wanafiki kwa kiwango cha juu sana. 

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search