Monday, 8 January 2018

Nairobi, Kenya: Tundu Lissu aituhumu Serikali ya Tanzania kwa jaribio la kutaka kumuua na Bunge kutomhudumia Matibabu

Kwa kirefu zaidi:


Kesho natimiza miezi minne tangu niletwe hapa Nairobi Hospital nikiwa sijutambui,nishukuru timu ya madaktari waliofanya kazi ya kuokoa maisha yangu".

Kwa namna ya kipekee kabisa niwashukuru wauguzi na madaktari wa Nairobi Hospital kwa kunifanya leo baada ya miezi minne niko hivi mnavyoniona.

Nilipigwa risasi 16 lakini mpaka sasa hakuna taarifa ya kukamatwa kwa mtuhumiwa yeyote wala sijahojiwa mbali na vitisho kwa Dereva wangu na kwa kifupi hakuna uchunguzi wowote kuhusu tukio hilo.

Kwa mara ya kwanza, kikundi cha watu wanaoitwa hawajulikani, walichukua bunduki za vita wakanifuata Bungeni, nilipotoka Bungeni mpaka nyumbani kwangu saa saba mchana kwa lengo la kuniua.

Kuna risasi moja nyuma ya uti wa mgongo. Madaktari wamesema ni hatari zaidi kuitoa kuliko ikibaki

Kilichofanyika dhidi yangu lilikuwa ni tukio la mauaji ya kisiasa moja kwa moja (Planned Political Assasination).

Sikupigwa Risasi za Bastola,walichukua bunduki za Vita wakanifwata kwa lengo la kuniua,ni kwa mara ya kwanza kutokea Tanzania.

Nilipigwa risasi 16 lakini mpaka sasa hakuna taarifa ya kukamatwa kwa mtuhumiwa yeyote wala sijahojiwa mbali na vitisho kwa Dereva wangu na kwa kifupi hakuna uchunguzi wowote kuhusu tukio hilo.

Jeshi la polisi kwa maoni yangu halipepelezi tukio hili kwa sababu wanajua njama za mauaji ya kisiasa kwa sababu nasumbua wakubwa wa Tanzania.

Serikali ya Tanzania na Jeshi la polisi lilifanya kila lililowezekana kuhakikisha watu hawalitaji jina la Tundu Lissu.

Haijawahi kutokea kwa mtu au kikundi cha watu kuchukua silaha na kwenda kumuua kiongozi wa kisiasa kwa sababu tu ya msimamo wake, hii ni mara ya kwanza katika historia.

Kosa kubwa la Tanzania ni kosa la uchochezi, ukiikosoa serikali ni mchochezi, ukimkosoa Rais ni mchochezi, ukimkosoa waziri ni mchochezi.

Sikushambuliwa na silaha za kawaida, nilishambuliwa na silaha za kivita.

Leo nazungumza hapa mbele yenu, Bunge la Tanzania halijatoa hata senti kumi kulipia gharama zangu za matibabu.

Serikali ambazo zina wajibu wa kulinda maisha ya raia wake, zinapoacha wajibu huo zinapaswa kuzomewa na dunia nzima.

Ni wakati wa vyombo vya habari kuihoji Serikali ya Tanzania.. Kwanini mnapiga watu risasi? Kwanini miili ya watu inapatikana ikielea baharini? Kwanini watu wanapotea?

Tangu nishambuliwe, Rais Magufuli hajasema chochote kuhusiana na tukio hili. nimeambiwa kuwa aliandika 'tweet', lakini siamini kama anaweza kutweet kama Rais Donald Trump.

Nimefanyiwa Oparesheni 17 na kwa sasa ninaweza kusema sio nimepata nafuu lakini nimepona kabisa.

Nashukuru Mwenyekiti wa CHADEMA kwa kunileta Nairobi. Serikali ilitaka nitibiwe Dar es Salaam ili niwe chini ya uangalizi wao mbovu.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search