Friday, 26 January 2018

NIKI WA PILI AMJIBU NASARI-ASEMA HATUJAMTENGA SUGU ILA WASANII HAWANA UMOJA

Nikki wa Pili Amjibu  Joshua Nassari " Hatujamtenga Sugu ila Wasanii Hawana Umoja"
Msanii kutoka kampuni ya Weusi, Nikki wa Pili amemjibu Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari kwamba si kweli kuwa wameamua kumtumikia 'kafiri' ila kimsingi wao hawana ufahamu wa kuongelea masuala ambayo bado yanaendelea Kimahakama.


Nikki amebainisha hayo wakati alipokuwa akifanya mahojiano na mwandishi wa habari hii baada ya Mbunge huyo kutoa lawama zake kwa wasanii katika ukurasa wake wa twitter asubuhi ya leo kutokana na kuwaona wapo kimya katika kesi inayomkabili Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi 'Sugu' ya kutoa maneno yenye kuleta chuki kati ya serikali na wananchi wakati alipokuwa katika mkutano wake wa hadhra ambao ulifanyika Disemba 31, 2017 jijini Mbeya


"Wasanii hawana umoja, chama chao hakina nguvu kwa hiyo hata kunapotokea jambo wasanii walitolee sauti kwa pamoja kuna hakuna 'platform' ya kushikilia jambo hilo na kujikuta kila msanii yupo peke yake, na kupaza sauti kila mtu peke yake wasanii wengi wanaogopa hilo", alisema Nikki wa Pili.

Pamoja na hayo, Nikki wa Pili aliendelea kwa kusema si jambo la kweli kama watu wanavyodhania kuwa tasnia ya muziki imemtenga Sugu ila tatizo lipo katika namna ya uwasilishaji wa jambo hilo.

"Hapana hatuwezi kumtenga Mhe. Sugu ila kuna jambo moja naweza kusema kwamba hili suala bado lipo kimahakama na tumeona wenyewe wamewaweka Wanasheria, kwa hiyo sisi wasanii bado hatuna ufahamu wa kujua jambo likiwa Mahakamani unaweza kulisema kwa upande gani kwa maana mara nyingi huwa tunaambiwa tusiingilie kazi za Mahakama", alisisitiza Nikki wa Pili.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search