Wednesday, 3 January 2018

NISHA AFUNGUKA MAZITO ASEMA MABWANA WALIMLIZA SANA MWAKA 2017

Nisha Afunguka Kuhusu Mapenzi 'Mabwana Waliniliza Mwaka 2017
STAA wa filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ ameibuka na kuelezea kufurahishwa kwake na kumalizika kwa mwaka 2017 kwani ulimliza na kumfunza mengi katika suala la mapenzi baada ya mabwana zake wawili kuporwa na mastaa wenzake.Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Nisha alisema kutokana na kufanyiwa kitendo hicho, mikakati yake mipya mwaka huu ni kumficha mpenzi wake.“Wapenzi wangu wawili nililizwa wapenzi wangu wawili na hii ni baada ya kuwaanika hadharani hivyo kwa sasa sifanyi tena hayo mambo ya kumwanika hivyo itakuwa ngumu kumuiba kwa sababu wengi wana hila wakishajua flani yupo na mimi ndiyo wananifanyia makusudi,” alisema Nisha.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search