Tuesday, 23 January 2018

Peter Msikwa Ashikiliwa na Polisi

Peter Msikwa Ashikiliwa na Polisi


Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano kutokana na matukio ya kiuharifu yanayotokea mjini Iringa.

Mbunge huyo anahojiwa kuhusu kuchomwa nyumba ya Katibu wa UVCCM na kuvunjwa Nyumba ya Diwani aliyehamia CCM akitokea CHADEMA.

Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa (RPC) Julius Mjengi ameuthibitisha kushikiliwa kwa Mchungaji Peter Msigwa ambapo ameeleza anahojiwa kuhusu  matukio ya uvunjwaji wa nyumba ya aliyekuwa diwani wa kata ya Mwangata kupitia chadema aliyejiuzulu na kujiunga na CCM pamoja na tukio la kuchomwa moto kwa nyumba aliyokuwa akiishi katibu wa UVCCM Iringa mjini.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search