Wednesday, 24 January 2018

POLISI : NABII TITO ANA TATIZO LA AKILI


Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amesema daktari wa Hospitali ya Mirembe mkoani humo amethibitisha kuwa Tito Machibya maarufu kwa jina la Nabii Tito ana tatizo la akili.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 23, mwaka 2018 baada ya kumkamata nabii huyo, Muroto amesema baada ya kumkamata leo wataendelea kumshikilia kwa ajili ya usalama wake kwa kuwa anajenga chuki dhidi ya dini za watu wengine wenye imani tofauti.

Amesema Nabii Tito alikamatwa na Polisi Januari 16, baada ya kuhojiwa alionekana kuwa na tatizo la akili na kuamua kumpeleka katika hospitali hiyo ya wagonjwa wa akili.


Amebainisha kuwa alipofanyiwa uchunguzi na daktari aliyemtaja kwa jina moja la Philipo alibaini kuwa nabii huyo ana tatizo hilo.

Nabii huyo amekuwa akionekana mitaani akihubiri huku akiwa anakunywa pombe.

Na Rachel Chibwete, Mwananchi

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search