Wednesday, 10 January 2018

Prof. Benson Bana: Tanzania inarudi kwenye Demokrasia pana, demokrasia ndani ya upinzani wa Tanzania imememinywa

bana.jpg ​

Dar es Salaam.

Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof. Benson Banna, mapema leo Jumatano Januari 10, 2018 amezungumzia masuala mbalimbali ikiwemo siasa hapa nchini.

Kwa mujibu wa mahojiano yake na kituo kimoja cha Televisheni hapa nchini, Prof. Banna ameonesha kushangazwa kwake na kitendo cha upinzani kudai katiba mpya, na kusema kuwa katiba mpya sio mwarobaini wa matatizo ya Watanzania badala yake waishauri serikali kutekeleza miradi ambayo itawaletea maendeleo Watanzania.

“Sioni kama katiba mpya ni mwarobaini wa matatizo ya mtanzania, sijui kama katiba itashughulikia suala la makinikia, sijui kama katiba itasimamia stigller (mradi wa umeme), sijui kama katiba itatujengea fly over” amesema.

Prof. Banna amedai kuwa kunaweza kuwa na katiba mpya, lakini pasipokuwepo na maamuzi ya dhati ya kusimamia katiba ile, inaweza kuwa ni maandishi mazuri tu kwaajili ya kusoma.

Akizungumzia suala la Demokrasia nchini, amesema kuwa kwa hali ya siasa inavyokwenda sasa nchini, ni dalili kwamba Tanzania inarudi kwenye Demokrasia pana. Amedai Tanzania iko miongoni mwa nchi tano bora mahiri kwa Demokrasia

Aidha amedai kuwa Demokrasia ndani ya upinzani wa Tanzania imememinywa sana, kiasi kwamba kunakuwa na kiongozi anatawala miaka 15, kana kwamba hakuna watu wengine wenye uwezo wa kuongoza

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search