Wednesday, 31 January 2018

Rais Trump atangaza 'enzi mpya ' kwa Marekani katika hotuba kwa taifa

Trump

Haki miliki ya pichaAFP
Image captionTrump amesema kuwa "yuko tayari kushirikiana " na Democrats kuweka kando mgawanyiko mkali wa kisiasa baina ya vyama hivyo
Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza "enzi mpya kwa Marekani" alipokuwa akitoa hotuba ya kitaifa kuhusu hali ya nchi Jumanne usiku.
Katika hotuba hiyo iliyotolewa kwa Bunge la Congress, aliwaambia wabunge kuwa: "Hapajawahi kutokea wakati mzuri wa kuanza kuishi ndoto za Marekani kama kipindi hiki."
Kiongozi huyo wa chama cha Republican amesema kuwa "yuko tayari kushirikiana" na Democrats kuweka kando mgawanyiko mkali wa kisiasa baina ya vyama hivyo.
Uchumi wa Marekani unakua kwa kasi, lakini umaarufu wa Bwana Trump umeendelea kushuka.
Katika hotuba yake iliyokuwa na kauli kali tofauti na wakati wa kuapishwa alipoonekana mwenye ghadhabu na kueleza "Marekani ilivyoharibiwa " mwaka mmoja tu uliopita , Bwana Trump amesema kuwa utawala wake "unajenga Marekani iliyo salama, thabiti na ya kujivunia ".
Watazamaji milioni 40 wa vituo vya vya televisheni inakadiriwa walimsikiliza akijaribu kuleta umoja wa kitaifa kama "timu moja, watu wamoja, na familia moja ya Waarekani".
Kuhusu sera ya kigeni, Bwana Trump anasema kuwa karibu maeneo yote ya Syria na Iraq ambayo wakati mmoja yalidhibitiwa na kundi la Islamic State yamerejeshwa tena.
Ameapa akisema: ''Tutaendelea na mapigano yetu hadi ISIS itakaposhindwa."

Democrat wamjibu Trump

Mjumbe wa Congress wa jimbo la Massachusetts Joseph Kennedy III, mpwa wa rais wa zamani wa Marekani John K Kennedy, atatoa mkakati wa Democrats wa kukabiliana na hotuba ya Bwana Trump.
Atajaribu kuiharibu hotuba ya Bwana Trump kwa kutaka kuongea kwa niaba ya: ''Wamarekani wanaohisi wamesahaulika na kutelekezwa".
Akielezea kusikitishwa kwake na " nchi iliyogawanyika" na kuuelezea urais wa Bwana Trump kama "fujo", Bwana Kennedy mwenye umri wa miaka 37, atasema: " katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita wengi wameishi maisha ya wasiwasi, hasira na uoga."
''Wadhalilishaji wanaweza kupata sifa," atasema. "Wanaweza kuacha historia.
Seneta wa Joseph Kennedy III
Image captionMbunge wa Massachusetts Joseph Kennedy III, mpwa wa rais John F Kennedy,alitoa hotuba ya kupinga hotuba ya rais kwa niaba ya Democrats
"Lakini hata wakati mmoja katika historia ya Marekani yetu hawataweza kuvunja uthabiti na moyo wa watu walioungana katika kulinda hali yao ya baadae."

Nyuso za hasira

Katika wakati mmoja , wajumbe wa chama cha Democratic weusi walikaa kimya kwa nyuso za hasira wakati wabunge wengine waliposimama kushangilia hotuba wakati Bwana Trump aliposema kuwa viwango vya Wamarekani weusi wasio na ajira vimeshuka kwa kiwango ambacho hakijawahi kurekodiwa .
Takriban wabunge kumi na wawili wa Democratic wanatarajiwa kupinga hotuba ya Bwana Trump katika kile ambacho kinaweza kuwa moja ya ususiaji mkubwa wa hotuba ya rais kwa taifa
Mmoja wao ni Mbunge wa Baraza la Congress jimbo la California Bi Maxine Waters, ambaye alikiambia kituo cha televisheni cha MSNBC: " Kwa nini nichukue muda wangu kwenda na kukaa kumsikiliza muongo?."

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search