Tuesday, 23 January 2018

Sanchez atua Manchester United

Alexis Sanchez atua Manchester

Image captionAlexis Sanchez atua Manchester
Zoezi la usajili kwa wachezaji Alexis Sanchez kwenda Manchester United na Henrikh Mkhitaryan kwenda Arsenal limekamilika, baada ya United kumtangaza rasmi Sanchez kuwa mchezaji wao na kwamba atakuwa akilipwa kitita cha paun 600,000.
Sanchez akitangazwa kuwa mchezaji mpya wa United, nyota huyo amesema anafuraha kuwa mchezaji wa kwanza kutoka Chile kuichezea klabu kubwa duniani.
Sanchez atakuwa anapokea mshahara wa Paun 350,000 kila wiki huku akipewa kiasi cha pauni 100,000 kupitia matangazo na pia atapewa nyongeza nyingine ya paun 140,000 kwa wiki.
Wakati Sanchez akitangazwa na Manchester United, naye mchezaji Henrikh Mkhitaryan ametangazwa na Arsenal kama mchezaji wao mpya, Mkhitaryan amesema kwenda Arsenal ndiyo zilikuwa ndoto zake tangu akiwa mtoto na alitamani siku moja kuitumikia Arsenal kupitia mkataba wa mabadilishano. Wakati huo huo Arsenal imepiga hatua katika kumwania mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang kutoka Borussia Dortmund.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search