Friday, 19 January 2018

Sanchez Kutambulishwa Manichester United

 Sanchez Kutambulishwa Manichester United Leo Apewa namba ya George Best
Mshambuliaji wa kimataifa raia wa Chile, Alexis Sanchez yupo tayari kutambulishwa na klabu ya Manchester United hii leo kama mchezaji halali wa timu hiyo huku akitarajiwa kupokea kitita cha paundi 450,000 kwa wiki.

Alexis akiwa na namba 7 ndani ya  United tayari mashabiki wameanza kumiminika katika duka la Adidas mtaa wa Oxford jijini London

Wakati utambulisho wa Sanchez ukingojewa tayari mashabiki wameshaanza kuvamia maduka na kujinunulia jezi ya mchezaji huyo ambayo ni namba 7 sawa na ile waliyokuwa wakivaa wachezaji wenye majina makubwa ndani ya United kama George Best, Eric Cantona, David Beckham na Cristiano Ronaldo. Na maduka ya Adidas yaliyopo mtaa wa Oxford jijini London.Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger hapo jana kupitia kikao chake na waandishi wa habari amethibitisha Sanchez wamemalizana na United.

Wenger amesema “Nimeufanyia kazi uhamisho kwa miaka sasa 30. Lakini kwa wakati wowote,dakika yoyote kunakitu kitashuhudiwa na hii ndiyo maana halisi ya usajili,”amesema Wenger.

Sanchez atakuwa akilipwa kwa wiki paundi 350,000  ukijumuisha na haki ya matangazo ambayo ni paundi 100,000  inakuwa jumla ya paundi 450,000. 

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search