Monday, 29 January 2018

Sumaye: Wanaojiuzulu nafasi zao hawatambui majukumu yao

Related image

Waziri Mkuu Mstaafu , Frederick Sumaye amefunguka na kusema kuwa kazi ya Mbunge ni kutetea wananchi wa jimbo lake na si kwenda kumsifia Rais na kudai wabunge waliojizulu nafasi zao kwa kigezo cha kumuunga mkono Rais hawakutambua majukumu yao.

Sumaye amesema hayo kwenye kampeni za Ubunge wa marudio katika jimbo la Kinondoni zinazoendelea na kusema kuwa kwa Wabunge ambao wamejiuzulu nafasi zao na kwenda chama kingine kugombea tena hawafai kabisa kuwa wabunge kwa kuwa hawatambui maana ya Ubunge.

"Kazi ya Mbunge si kwenda kumtetea Rais bali ni kutetea wananchi waliompa kura, kama Mtulia yeye anasema ameondoka na kudharau kura za watu wa Kinondoni kwa sababu amependezeshwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania basi akateuliwe na Rais kuwa Mbunge maana kazi yake ndiyo itakuwa kwenda kumtetea na kumsifia Rais. 

Watu ambao wanahama chama eti kwa sababu Rais ametenda mambo mema pamoja na ukweli kwamba mimi naweza kubishana sana maana hatujaona hayo mambo wewe kama umehama maana yake ulikuwa uelewi maana ya kuwa Mbunge" alisisitiza Sumaye
Mbali na hilo Sumaye alidai kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa sasa hakijali tena maslahi ya wananchi wake kwa kuwa kimeshika madaraka kwa muda mrefu ndiyo maana wameweza kumrudisha Mtulia kugombea kwenye jimbo la Kinondoni bila kujali mtu huyo amesababisha fedha za wananchi zaidi ya bilioni moja ziteketee kwenye uchaguzi wa marudio wakati fedha hizo zingeweza kutumika katika kufanya mambo ya maendeleo kwa wananchi

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search