Wednesday, 31 January 2018

Tetesi za soka Ulaya Jumatano 31.01.2018

Daley Blind

Image captionRoma inamuwinda mchezaji wa Manchester United mholanzi Daley Blind
Roma inawasilisana na Manchester United kumhusu beki wa Uholanzi Daley Blind mwenye umri wa miaka 27. (Mirror)
Viongozi wa ligi ya Serie A Napoli wameanzisha mazungumzo na Everton kwa azma ya kusaini mkataba na mchezaji wa kati Mholanzi Davy Klaassen, mwenye umri wa miaka 24, kwa mkopo hadi kufikia mwishoni mwa msimu. (Liverpool Echo)
Meneja wa Newcastle Rafa Benitez amefanya mazungumzo ya dharura na mmiliki Mike Ashley na bado ana ''matumaini'' ya kusaini mkataba kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kuhama wachezaji baadaye leo. (Mirror)
Lakini Benitez anasisitizia msimamo wake ambao hautarajiwi kubadilika hata kama itashindikana kuhama kwa washambuliaji anaowalenga kama Islam Slimani na mlinzi wa Manchester City Eliaquim Mangala (Northern Echo)
Ovie Ejaria,
Image captionMchezaji wa kiungo cha kati wa Liverpool Ovie Ejaria anataka kujiunga na Sunderland
Arsenal itamruhusu mlinzi Mathieu Debuchy, mwenye umri wa miaka 32, kujiunga na Saint-Etienne kwa uhamisho wa bila malipo. (L'Equipe - in French)
West Ham imezungumza na Lille kuhusiana na mpango wa kusaini mkataba na nahodha wao Ibrahim Amadou.
Crystal Palace wamekwishatoa mapendekezo mawili kwa ajili ya mlinzi huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 24. (Sky Sports)
Wolfsburg wanajaribu kumshawishi mchezaji kiungo wa kati wa kimataifa wa Serbia anayechezea Liverpool Lazar Markovic, mwenye umri wa miaka 23, kujiunga nao kuliko kwenda klabu ya Swansea. (Mail)
Kiungo wa kati wa Liverpool Ovie Ejaria, mwenye umri wa miaka 20, yuko tayari kujiunga na Sunderland kwa mkopo kwa kipindi kilichosalia cha msimu pamoja na mkabaji Mwingereza Lloyd Jones, mwenye umri wa miaka 22, anayetaka kuhama na kuwa mchezaji wa kudumu wa Luton Town . (Liverpool Echo)
Leeds United wanakamilisha taratibu za kusaini mkataba na mshambuliaji Tyler Roberts kutoka West Brom katika mkataba wenye thamani ya hadi £4m. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 19 kutoka Wales ana miezi sita iliyosalia kwenye mkataba wake wa sasa. (Mail)
Nicklas BendtnerHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBendtner anaweza kusaini mkataba wa awali na klabu ya Ufaransa ya Bordeaux
Mazungumzo ya Swansea na West Ham yamefikia kiwango kikubwa kumleta mshambuliaji wa Ghana Andre Ayew mwenye umri wa miaka 28 katika uwanja wa Liberty, lakini wamechelewa kusaini mkataba na mchezaji huyo, pamoja na kiungo wa kati wa Korea Kusini Ki Sung-yueng, mwenye umri wa miaka 29 . (Wales Online)
Bordeaux wako katika mazungumzo na raia wa Norway anayechezea Rosenborg kwa ajili ya kutia saini mkataba na mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Nicklas Bendtner. Bendtner mwenye umri wa miaka 30 anaweza kusaini mkataba wa awali na klabu hiyo ya Ufaransa. (TalkSport)
Baada ya kumnunua beki wa Ufaransa Aymeric Laporte kutoka Athletic Bilbao, pesa walizotumia Manchester City kuwanunua wachezaji zimezidi bajeti ya ulinzi ya mataifa 52. (i News)
Mipango imetangazwa ya kutengeneza filamu ya maisha ya mshambuliaji wa zamani wa Everton Dixie Dean, ambapo Toby Kebbell anatarajiwa kuongoza shughuli hiyo. (Liverpool Echo)
Uingereza inaweza kuwa na timu ya soka ya wanawake katika michuano ya Olimpiki ya 2020 baada ya timu nne za nyumbani kufikia mkataba. (Mail)

Kutoka Jumanne

Tottenham watamruhusu mshambuliaji Fernando Llorente ajiunge na Chelsea iwapo tu watapata faida kubwa juu ya £14m walizolipa kumnunua mchezaji huyo wa Uhispania Septemba. (Evening Standard)
Chelsea watakataa ofa zozote kutoka kwa Manchester City kutaka kumnunua mchezaji wa Ubelgiji Eden Hazard, 27, hata kama Pep Guardiola na klabu yake wako tayari kuvunja rekodi ya dunia ya ununuzi wa wachezaji ya £200m. (Telegraph)
West Brom wanaongoza katika juhudi za kumtaka mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Ujerumani Andre Schurrle, 27, ambaye pia anatafutwa na West Ham. (Teamtalk)
Juventus wana matumaini makubwa ya kumnunua mchezaji wa safu ya kati kutoka Ujerumani anayechezea Liverpool Emre Can, 24, ambaye mkataba wake utamalizika mwisho wa msimu huu. (Mail

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search