Monday, 8 January 2018

TRA: Makusanyo ya Mwezi Dec 2017 yamepanda hadi trilioni 1.66 sawa na ongezeko la ukuaji wa 17.65%

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeeleza kuwa kwa mwezi July hadi December kwa Mwaka wa Fedha 2017/18 imekusanya Tsh Trilioni 7.87 ikilinganishwa na Tsh Trilioni 7.27 ya kipindi hicho hicho kwa mwaka wa fedha 2016/17 ikiwa ni ongezeko la 8.46%.

Mamlaka hiyo kwa mwezi Desemba 2017 pekee, imekusanya jumla ya tsh trilioni 1.66 ambapo ni ongezeko la ukuaji wa 17.65% ikilinganishwa na kiasi kilichokusanywa mwezi Desemba mwaka 2016 ambapo TRA ilikusanya tsh trilioni 1.41

TRA.jpg

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search