Wednesday, 3 January 2018

TRUMP AMJIBU KIM JON -UN KIBONYEZO CHANGU CHA NYUKLIA NI KIKUBWA NA KINA NGUVU KULIKO CHA KIM

Rais wa Marekani Donald Trump amejigamba kuwa kibonyezo chake cha silaha za nyuklia ni kikubwa na kilicho na nguvu zaidi kuliko kile cha kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jon-un.

Ujumbe wa Twitter wa Trump ndiyo wa hivi punde wakati ya majibizano kati ya viongozi wa mataifa hayo mawili yaliyo na silaha za nyukilia.

Mapema wiki hii Kim alionya kuwa kibonyezo chake cha nyuklia kawaida kiko kwenye meza yake.

Korea Kaskazini inadai kuwa ina silaha za nyulia na inaweza kuishambulia Marekani huku wadadisi wakisema kuwa ikiwa Korea Kaskazini ina silaha za nyulia haibainiki ikiwa ina teknolojia ya kuzitumia.

Kando na kuitishia Marekani, ujumbe wa mwaka mpya wa Kim pia uliwashangaza wengi wakati alisema kuwa alikuwa aayari kwa mazungumzo na Korea Kusini na angependa kuituma timu kwa mashindano ya olimpiki ya msimu wa baridi nchini Korea Kusini mwezi ujao.

Chanzo-BBC

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search