Wednesday, 3 January 2018

VITUO KADHAA VYA RUNINGA VYA RUNINGA VYATOZWA FAINI NA TCRA

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania, TCRA, imevipiga faini vituo vitano vya Televisheni kwa makosa ya ukiukwaji wa taratibu za kutangaza taarifa ya habari hapa nchini.

Adhabu hiyo imetangazwa leo na Makamu mwenyekiti wa kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) , Joseph Mapunda


Kituo cha runinga cha EATV, kimetozwa faini ya jumla ya TZS milioni 15, kwa makosa matatu ikiwemo, kukiuka maadili ya uandishi na kutangaza habari za uchochezi. Faini hiyo inapaswa kulipwa ndani ya siku 30, na kituo hicho kitawekwa chini ya uangalizi kwa muda wa miezi 6.


Aidha, TCRA imekitoza faini ya TZS milioni 15 kituo cha Runinga cha Channel ten, kwa makosa ya kutangaza habari ambazo hazikuzingatia maadili ya uandishi, kutangaza habari za uchochezi, na kutozingatia mizania. Pia kituo hicho kitawekwa chini ya uangalizi kwa miezi sita kuanzia leo.


Kituo cha runinga cha Star TV, kimetozwa faini ya jumla ya TZS milioni 7.5 kwa makosa matatu ikiwemo, kukiuka maadili ya uandishi na kutangaza habari za uchochezi. Faini hiyo inapaswa kulipwa ndani ya siku 30 na pia kituo hicho kinawekwa chini ya uangalizi wa miezi 6.


Pia TCRA imekitoza faini ya TZS milioni 7.5 kituo cha runinga cha Azam Two, kwa makosa ya kutangaza habari za uchochezi, kutangaza habari ambazo hazikuzingatia maadili ya uandishi na kutozingatia mizania. Pia kituo hicho kitawekwa chini ya uangalizi kwa miezi sita kuanzia leo. 

Kituo cha runinga cha ITV, kimetozwa faini ya jumla ya TZS milioni 15, kwa makosa matatu ikiwemo, kukiuka maadili ya uandishi na kutangaza habari za uchochezi. Faini hiyo inapaswa kulipwa ndani ya siku 30, na kituo hicho kitawekwa chini ya uangalizi kwa muda wa miezi 6.
Soma mashauri haya kwa undani hapa chiniUamuzi kuhusu shauri namba 4 la mwaka 2017/18 dhidi ya Star Television. 

Kupitia kipindi chake cha taarifa ya habari kilichorushwa kati ya saa mbili usiku kikisema kuwa uchaguzi ulikuwa na uvunjifu wa haki za binadamu juu ya vyombo vya dola

Kwa kurusha taarifa hiyo kituo cha Star Television kinatuhumiwa kukiuka sheria zifuatazo;
  • Kutangaza habari za uchochezi zinazoweza kuhatarisha amani ya nchi na taifa kinyume na kanuni za utangazaji za mwaka 2015
  • Kukiuka maadili ya uandishi kwa kutangaza habari zisizokuwa na mizania na kinyume ya kanuni ya utangazaji
Sehemu ya habari hiyo ya StarTv ni hii hapa kwa nukuu "Mwenyekiti wa chama Chadema tawi la Dar es Salaam, ndugu Dikson ambaye alijeruhiwa vibaya sana na kuonekana kuwa amelazwa katika wodi kwa sababu ya uchaguzi, Picha ya chini tunaona mawakala wa chadema wa Arumeru ambao alishambuliwa na mapanga wakiwa wanatimiza wajibu wao"

"Ukiukwaji huo wa haki za binadamu umehusihwa kupigwa kwa binadamu na kukamatwa kwa baadhi ya viongozi wa kisiasa pamoja na kubuguziwa kwa mawakala mbalimbali. Kumekuwa na vitendo vya matumizi mabaya ya nguvu na vyombo vya dola, matukio ya watu kutwekwa na watu wasijulikana, watu kupigwa na vitendo hivi vimeripotiwa kufanywa na vyombo vya dola na watu wasiojulikana wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa vyama vya siasa"

Wito wa kufika kwenye kamati ya maudhui
Tarehe 5/12/2017 uongozi wa Star Tv uliitwa kutoa utetezi kwanini wasichukuliwe hatua kwa kukiuka kanuni za utangazaji;

Baada ya kuwaita, kamati na hao viongozi ilipata nafasi ya kutazama kipindi ili kujua kama ilikiuka kanuni za utangazaji.

Uongozi wa Star Tv ulitoa utetezi kama ifuatavyo:
1.Vyombo vya habari vya habari vilikaribishwa kwenye mkutano wa kituo cha sheria na haki za binadamu kwa lengo la kuzungumzia tathmini ya uchaguzi mdogo.

2.Walisikitishwa na taarifa iliyotolewa na taasisi ya kituo cha sheria na haki za binadamu, taarifa hiyo ilikuwa na makosa lakini mhariri wa zamu hakuyaona na kwamba hakupaswa kutangazwa bila kuifanyia marekebisho.

3.Star Tv walishachukua hatua za ndani kwa mhariri ili kuhakikisha suala hilo halijirudii.

4.Star Tv walieleza kuwa si tu kuwa taarifa hiyo ilikiuka kanuni za utangazaji bali ilikiuka sera ya kituo chao.

Star Tv waliomba radhi kwa taarifa isiyozingatia kanuni za utangazaji

Star Tv wamekiuka kanuni namba sita ya kanuni ya utangazaji;
Pamoja na kwamba taarifa hiyo ilikuwa inaihusu tume ya uchaguzi hawakuwasiliana na tume ya uchaguzi kupata undani wa taarifa hiyo. Pia hawakuwasiliana na jeshi la polisi ili kupata mizania ya habari hiyo.

Kamati imeitazama taarifa hiyo na utetezi wa Star Tv

Pamoja na kukiri kutenda kosa, kamati imejiridhisha kuwa imekiuka kanuni za utangazaji za mwaka 2015.

Baada ya kubaini makosa hayo, kamati ya maudhui inaamua yafuatayo

1.Star Tv inatozwa faini ya shilingi milioni 2 na nusu kwa kosa la kutangaza habari za uchochezi.
2.Star Tv inatozwa faini ya shilingi milioni 2 na laki tano kwa kutangaza kanuni za utangazaji.
3.Kwa kutozingatia mizania ya habari Star Tv inatozwa shilingi milioni 2 na laki 5

Kwa makosa yote Star Tv inatozwa shilingi za kitanzania milioni 7 na laki 5
Faini hiyo inatakiwa kulipwa ndani ya siku 30. Pia Star Tv inawekwa chini ya uangalizi maalum wa TCRA.
Uamuzi huu umetolewa leo tarehe 2/01/2017

Sasa tunasoma uamuzi unaohusu shauri namba sita mwaka 2017/18 unaohusu azamu two.

Kituo cha azam two, kinatuhumiwa kukiuka kanuni za utangazaji katika kipindi cha tarehe 30/11/2017.
=>Kilitangaza tathmini ya kituo cha sheria za haki za binadamu. Kwa kurusha taarifa hiyo, kutuo cha azam two kilikiuka kanuni zifuatazo;

Wito wa kufika mbele ya kamati ya maudhui

Azam two waliitwa mbele ya kamati ya maudhui ili wajitetee kwanini wasichukuliwe hatua

Malelezo ya azam

=>Walikiri na kukubali kutangaza habari hiyo
=>Kwa ujumla waandishi walijitahidi kwa uwezo wao kupata maelezo ya ziada kutoka tume ya uchaguzi lakini hawakufanikiwa. Kutokana na hili ndipo walipofanya uamuzi ambao haukuwa wa busara.

=>Ilikuwa imeandaliwa mkurugenzi atoe ufafanuzi lakini hakuwa tayari maana alikuwa kwenye mkutano.

=>Azam two waliahidi kuhakikisha waandishi wao wanazingatia weledi kwa kuweka uzalendo mbele.

Azam two;

Nimalizie kwa kukuomba radhi wewe na kamati yako

Kwa kuzingatia azam two wametenda makosa, kamati imeamua yafuatayo;

1.Azam inatozwa milioni 2 na laki 5 kwa kutangaza habari za uchochezi
2.Azam two inatozwa milioni 2 na laki 5 kwa kutangaza habari zisizozingatia maadili
3.Kwa kutozingatia mizania azam two inatozwa milioni 2 na laki 5.

Jumla azam two inatozwa jumla ya shilingi milioni 7 na laki 5

Pia azam two inawekwa chini ya uangalizi maalum wa TCRA kwa miezi 6


Uamuzi huu umetolewa na kusomwa leo tar 02/01/2018

Shauri kuhusu kituo cha East Africa Television

Kamati imeangalia maelezo ya East Africa Televisheni
Pamoja na kutokiri kutenda kosa, kamati imejiridhisha, kituo cha East Africa Television kimekiuka kanuni za huduma za utangazaji.

Uamuzi wa kamati
Kamati ya maudhui imejiridhisha kipindi cha Hotmix kimekiuka kanuni za utangazaji na imeamua yafuatayo;

1. EATV inatozwa faini ya sh milioni 5 kwa kutangaza habari za uchochezi
2. EATV inatozwa faini ya sh milioni 5 kwa kutangaza habari zisizozingatia maadili
3. EATV inatozwa faini ya sh milioni 5 kwa kutozingatia mizania ya utangazaji.

Jumla EATV inatozwa faini ya milioni 15, faini inapswa kulipwa ndani ya siku 30

Pia EATV inawekwa chini ya uangalizi wa TCRA kwa miezi 6

Shauri namba tano mwaka 2017/18 kuhusu kituo utangazaji wa channel ten

Kituo cha utangazaji cha channel ten kinatuhumiwa kurusha taarifa inayokiuka kanuni za utangazaji.

Kituo cha channel ten kilirusha habari ya kituo cha haki za binadamu tathmini ya kituo cha sheria na haki za binadamu.

Utetezi wa channel ten ni kwamba ilitolewa na taasisi iliyosajiliwa.Pili tathmini ya kituo cha sheria na haki za binadamu ililenga kuutahadharisha umma. Channel ten wanasema taarifa hiyo ilikuwa na ushahidi wa picha. Nne kituo cha sheria na haki za binadamu ni chombo kilichosajiliwa kisheria nchini.

Katika kutoa majumuisho yao channel ten walisema kamati ipokee utetezi wao na kusitisha kusudio la kuichukulia hatua.

Kutokana na tathmini na baada ya kusikiliza uetetezi, kamati ya maudhui imejiridhisha chanel ten imekiuka kanuni za utangazaji;

Kamati imetoa uamuzi ufuatao;

1. Channel ten inatozwa sh milioni 5 kwa kosa la uchochezi
2.Channel ten inatozwa faini ya milioni 5 nyingine kwa kuzingatia kanuni za uandishi
3. Kwa kosa la kutozingatia mizania channel ten inatozwa sh milioni 5 pia.

Faini inatakiwa kulipwa ndani ya siku 30, pia channel ten inawekwa chini ya uangalizi kwa miezi 6.

Uamuzi kuhusu shauri namba tatu la mwaka 2017/18 la kituo cha utangazaji cha ITV;
Kituo cha ITV kinatuhumiwa kurusha habari za uchochezi kilichorushwa tarehe 30 Nov 2017. Kilirusha habari za kituo cha sheria na haki za binadamu kuhusu tathmini ya uchaguzi mdogo.

Utetezi wa ITV;
1. ITV walithibisha kutangaza habari hiyo tarehe 30 Nov 2017, walisema ililenga kuthibiti uwezekano wa kutokea vurugu.

2. Madhui hayakuwa ya uchochezi na Habari hiyo haikulenga kutokea vurugu.

3. Maadili ya uandishi yalizingatiwa na hakukuwa na taarifa ya Jeshi la polisi au tume ya uchaguzi kukanusha.

4. Taarifa ililenga kuishauri serikali

5.Walijiridhisha kuwa lengo kuu la tamko na kauli zilizotolewa hazikuwa za uchochezi

6. Walihakiki na kujiridhisha kuwa taasisi hii imesajiliwa kisheria.

Katika kujumuisha utetezi wao ITV walisema;
Taarifa ililenga kuishauri serikali, ilizingatia mizania na kwamba kituo chao hakikukiuka kanuni za utangazaji.

Kamati ya maudhui inaamua yafuatayo.

1.ITV inatozwa faini ya sh milioni 5 kwa kutangaza habari za uchochezi
2.ITV inatozwa faini ya sh milioni 5 kwa kutangaza habari ambazo hazikuzingatia maadili ya uandishi
3.Kwa kutozingatia mizania ITV inatozwa faini ya shilingi milioni 5

Kwa makosa yote ITV inatozwa faini ya sh milioni 15 kwa makosa yote matatu.
Faini hiyo inapaswa kulipwa ndani ya siku 30.

Haki ya kukata rufaa kwenye baraza la kibiashara uko wazi.

Kwa vile haya masuala ni ya kisheria haturuhusu maswali, ndiyo maana hapa tumeweka kipengele kwamba watu wana haki ya kukata rufaa, tukianza kuuliza maswali tutaingilia mkondo wa kisheria.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search