Friday, 5 January 2018

Wachezaji Wanne Waongezewa Mkataba Manchester United

WachezajiWanne Waongezewa Mkataba Manchester United


Klabu ya soka ya Manchester United wamewaongezea mikataba wachezaji wake wanne ambao mikataba yao ilikuwa inafikia ukingoni.Wachezaji hao ambao wameongezewa mikataba hiyo ni Juan Mata, Ander Herrera, Ashley Young na Daley Blind hadi mwisho wa msimu ujao. Wachezaji hao walikuwa wanatakiwa kuondoka bure mwishoni mwa msimu huu lakini United wamewapatia mikataba ya haraka wachezaji hao na kuimarisha ya maadili yao ya uhamisho kwa kuanzisha vifungu vinavyoongeza mikataba yao kwa miezi 12 hadi Juni 2019.

Mchezaji mwengine ambaye anatajwa kutaka kuongezewa mkataba ni Luke Shaw ambaye amewavutia sana mashabiki wa United kutokana na uwezo wake katika wiki za hivi karibuni na inawezekana kupewa mpaka mwisho wa msimu kuthibitisha thamani yake kabla ya uamuzi kufanywa juu yake.Hata hivyo Marouane Fellaini amekataa kuongeza mkataba mpya na timu hiyo ambapo mwishoni mwa msimu huu atakuwa huru na timu ya Besitkas inaongoza katika mbio za kutaka kumsajili kiungo huyo wa Ubelgiji.

Mourinho hataki kumuuza Fellaini katika dirisha la uhamisho la majira ya baridi na amejiandaa kumpoteza wakati wa majira ya joto. licha ya matatizo yake ya sasa ya kuumia. Fellaini ameanza mechi moja tu tangu mwisho wa Septemba kwa sababu ya kuumia.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search