Thursday, 11 January 2018

WAKILI KIBATALA AJITOA KESI YA WEMA SEPETU


Wakili Peter Kibatala ameiandikia barua Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akiomba kujitoa kumuwakilisha msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu katika kesi ya dawa za kulevya inayomkabili.


Hatua hiyo imekuja leo Jumatano, baada ya shauri lililopita Desemba 12, mwaka jana, mahakama hiyo kuelezwa kuwa wakili wa Wema hajafika na kushindwa kuendelea kusikiliza kesi hiyo.


Mbali na wakili Kibatala kuomba kujitoa katika kesi hiyo, mahakama hiyo imepokea barua kutoka kwa Wakili Albert Msando kuomba kumuwakilisha Wema katika kesi hiyo na kwamba aliomba apewe muda wa kupitia jalada hilo kabla ya kuendelea na kesi.


Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba anayesikiliza shauri hilo, amesema kuwa amepokea barua hizo Januari 9, mwaka huu na kuahirisha kesi hiyo hadi Februari 8, mwaka huu, itakaposikilizwa.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya kutumia dawa za kulevya ni Angelina Msigwa na Matrida Abbas.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search