Tuesday, 2 January 2018

Wananchi wana hali ngumu ya maisha – Mhe. Freeman Mbowe

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe. Freeman Mbowe amesema kuwa maisha ya Watanzania yamekuwa magumu kuliko katika kipindi chochote katika historia ya Tanzania.

 Mhe. Mbowe amesema hayo leo jumapili Desemba 31, 2017 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Waandishi wa Habari.

“Sio siri maisha ya wananchi yamekaza, mimi nimezunguuka nchi hii mikoa mingi, Wananchi wana hali ngumu ya maisha kuliko kipindi chochote katika historia ya nchi yetu,“amesema Mhe. Mbowe huku akifafanua kauli ya kupigwa marufuku kwa matumizi ya neno la vyuma vimekaza.

“Bwana mkubwa hataki neno hili kutumika anasema neno Vyuma vimekaza hataki litumike, Bwana mkubwa yeye vyuma vyake havijakaza kwa sababu halipi umeme, halipii nyumba ya kulala kwa sababu anafanyiwa kila kitu na serikali kwa kodi zetu.“amesema Mhe. Freeman Mbowe

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search