Friday, 26 January 2018

Waziri Selemani Jafo: Bilioni 660 zimetolewa na Serikali kuboresha Jiji la Dar es Salaam

Image result for suleiman jafo
Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh elemani Jafo amesema serikali imetoa Takribani Bilion 660 kuboresha Jiji la Dar es Salaam.

Waziri huyo amesema kuwa kupitia ofisi hiyo ndipo wananchi wanaweza kupata huduma mbalimbali, Watanzania wanafahamu kuwa Jiji la Dar es Salaam kwa muda limekuwa na changamoto ya usafiri.

Amesema mwanzo walianza na mradi wa mwendokasi ambao kwa sasa unafanya vizuri ila sasa kwa kuimarisha jiji la Dar es Salaam wamejikita katika mradi wa DMDP ili waeweze kufanya vizuri na kuboresha miundo mbinu ya Jiji la Dar hivyo wanamkakati wa kujenga barabara za lami zenye urefu wa kilomita 210.

Barabara hizo zitajengwa katika Manispaa tatu ikiwa ni Kinondoni, Temeke na Ilala. Mradi huu utagharibu kiasi cha dola milioni 300 kwa pesa za kitanzania ni bilioni 660 na mradi huo utatekelezwa hadi 2020 na utakuwa umekamilika.

Mradi huo pia utahusika na ujenzi wa barabara za lami, mifereji ya km 40 madaraja, lakini wataangalia zaidi mazingira ya Bonde la Msimbazi maana limekuwa changamoto kwa wananchi hivyo litachimbwa na kuboersha.

Watajenga masoko, yapatayo tisa na masoko hayo yatakuwa ya kisasa ili kuwezesha wananchi kuuza bidhaa zao.

Pia watajenga stendi,hivyo watafuata stendi zilizojengwa kiholela katika kata 12. kata zitawekwa barabara ili zipitike vizuri Ajenda ni kufanya jiji liwe la kisasa. Pia kutakuwa na barabara zitakazolisha barabara za mwendokasi.

Watanunua mitambo ya kukusanya taka na madampo ya kisasa na yatawekwa Arusha, Tanga, Mbeya.

Waziri huyu amesema kuwa anahitaji kuona value for money kwa kila litakalofamyika na amewaagiza wakurugenzi kuwa hataki masihara katika mradi huo na amewataka waratibu kuwa wasiwe watu wa kukaa ofisini.

 v

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search