Monday, 29 January 2018

Wema Sepetu-Nilipigiwa Simu na Nasbu ‘Diamond’ Akaniomba Nikamkubalia

“Nilipigiwa Simu na Nasbu ‘Diamond’ Akaniomba Nikamkubalia- Wema Sepetu
MSANII wa filamu Bongo, Wema Sepetu amefunguka kuwa alipigiwa simu na X wake ambaye ni Diamond Platinumz akimuomba afike Hyatt Regency Hotel kwa ajili ya kujumuika na watu wengine kwenye hafla ya kumtambulisha msanii mpya wa WCB, Maromboso ambapo hafla hiyo ilifanyika usiku wa kuamia leo.“Nilipigiwa simu na Nasbu ‘Diamond’ akaniomba nije kwenye hafla ya kumtambulisha msanii wao mpya wa WCB, nikakubali nikamwambia haina shida nitakuja, akaniuliza idadi ya watu nitakaokuja nao nikamwambia nitafika na marafiki zangu na timu yangu. Hivyo nimefurahi leo kujumuika na WCB kuwapa kampani,” alisema Wema.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search